Header Ads

Header ADS

Mkuu wa Wilaya ya Makete ahamasisha Wananchi kuchangia Maendeleo

Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Veronica Kessy ametoa wito kwa wananchi wanamakete wanaoishi ndani na Nje ya wilaya ya Makete kurudi nyumbani na kufanya maendeleo katika wilaya yao,kutokana na wanamakete wengi walio na vipato nchini kuwekeza  nje ya wilaya yao.
     Pia Veronica Kessy ametoa wito huo wakati akizindua mashindano ya M.D.A super cup  yaliyofanyika uwanja wa saba saba mjini Makete yaliyoanzishwa na chama cha maendeleo Makete M.D.A  kwa lengo la kuhamasisha maendeleo na kutambulisha chama hicho wilayani humo kilicho chini ya wajumbe/wanamakete wanaoishi ndani na nje ya wilaya hiyo.
  
“Hali niliyoiona wakati naingia Makete kwa kweli nikasema inatakiwa tufanye iwe wilaya ya kiutalii kwasababu wananchi wake,wamekuwa wamekuwa ni wakuhama na kwenda kufanya makazi maeneo ya nje ya Makete,nikawapa kazi M.D.A wahakikishe wenyewe waliopo nje ya Makete wanaludi Makete na kufanya maendeleo mbali mbali kwasababu tunaushahidi wa kutosha matajiri wakubwa waliopo Dar es salaam kariakoo,waliopo Makambako.Mbeya,Tunduma wote ni wanamakete lakini nyumbani kunafanana na huko?”anasema Veronica Kessy.
  Kwa upande wake  Katibu wa chama cha maendeleo Makete ndugu Award Mpandila anasema moja ya malengo ya chama hicho ni kuhamasisha jamii na watu wanao toka katika wilaya hiyo na kushindwa kukumbuka kuleta maendeleo.

“Malengo mojawapo ya chama chetu ni kuhamasisha jamii ya wanamakete ambao wakienda kuishi nje hawakumbuki nyumbani na wakileta maiti wanalala kwenye gari tumesema hiyo imetosha”anasema Mpandila.
Festo Richard Sanga ni mkurugenzi wa timu ya Singida United na mwenyekiti wa kamati ya michezo ya chama cha maendeleo Makete ambaye ameongozana na timu ya Singida United na kushiriki katika uzinduzi wa ligi ya M.D.A kwa kucheza na timu mbili wilayani humo.Amesema malengo yake ni kuona anapata vipaji kutoka Makete na tayari baadhi ya viongozi wa timu Singida United pamoja na viongozi wa wilaya wako macho kuangalia vipaji katika mashindano hayo.

Baadhi ya wananchi wilayani Makete wametoa pongezi kwa wanamakete wanaoishi nje ya wilaya yao kwa kuanza kuonyesha nia ya kulejesha maendeleo huku wakiomba chama cha maendeleo Makete kuongeza nguvu ili kumfikia kila mwanamakete aliyepo nje ya wilaya hiyo.

No comments

Powered by Blogger.