Header Ads

Header ADS

Naibu Waziri Wa Maji Amsimamisha Kazi Mhandisi Baseki Kwa Kuihujumu Serikali

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Mhandisi Leonard Baseki kwa kuihujumu serikali na kushindwa kukamilisha mradi wa maji Mkuranga.

Akizungumza baada ya kupata taarifa ya mradi wa maji Mkuranga, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara kufuatilia suala hilo na kumsimamisha kazi mhandisi huyo kwa kuihujumu serikali.
IMG-20191102-WA0031
Aweso amesema, mhandisi wa maji Baseka ameshindwa kutekeleza mradi huo na kuishia kuihujumu serikali zaidi ya Bilion 2 kwa kujenga mradi ambai hauna chanzo cha maji.

" Haiwezekani mhandisi tena wa serikali anaharibu hapa Mkuranga halafu anahamishiwa sehemu nyingine na kule anaenda Kuharibu pia kwahiyo nimemuagiza Katibu Mkuu amsimamishe kazi na apelekwe kwenye bodi ya wahandisi," amesema.

Aweso amesema, tayari wahandisi 95 wameshaondolewa kutokana na kutokukamilisha miradi na kuiingiza serikali  hasara na kuchelewesha adhma ya serikali ya kumtua mama ndoo kichwani

"Nawaonya wahandisi wengine kuwa hatutafumbia.macho pindi wanapohujumu Serikali tutawachukulia hatua ikiwemo kuwapeleka mbele ya kamati ya maadili," amesema

Akizungumzia mradi wa maji wa Mkuranga unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA, Aweso amemtaka Mkandarasi wa mradi huu kwenda kwa haraka ili wananchi wapate maji kwa wakati kama makubaliano yalivyo kwenye mkataba.

Aidha, Aweso amesema amewaagiza  DAWASA kufanya kikao cha pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Mkuranga na kufanya usanifu wa mradi wa Maji ili wakazi wote wa Mkuranga wapate maji.

"Nawapongeza DAWASA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendesha miradi, kwa fedha zao za ndani hili ni jambo kubwa sana tumeona Dar es Salaam wamefanya kazi na sasa wameamua kuja Mkuranga ili wananchi mpate maji safi na salama," amesem Aweso.

Hata hivyo,Aweso ameendelea na ziara yake ndani ya Mkoa wa Pwani wa kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama ili kuweza kumtua mama ndoo kichwani.
IMG-20191102-WA0035
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mkuranga kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Bakari Mgaya alipofika kulikagua tanki la maji lililopo kwenye hatua ya uienzi litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milion 1.5 na kuhuhudumia wakazi 25,000 kwa siku Mkuranga Mkoani Pwani

No comments

Powered by Blogger.