Novemba 15,2019 bunge linatarajia kupitisha mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya itakayowawezesha watu kujipima virusi vya ukimwi wenyewe.
Serikali imesema Novemba 15, 2019 Bunge linatarajia kupitisha mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya itakayowawezesha watu kujipima virusi vya ukimwi wenyewe.
Waziri wa afya,maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo Novemba 11,2019 wakati wa hufunguzi wa semina elekezi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), kwa wasanii mbalimbali jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin William Mkapa.
Aidha,amesema sheria iliyokuwepo awali ilikuwa hairuhusu watu kujipima wenyewe ila sasa itakuwa rasmi kabla ya Novemba 15,2019 kwani sheria hiyo itakuwa imepita na wananchi sasa wataweza kujipima virusi vya ukimwi wenyewe.
Pia,amesema, kipimo hicho hakitakuwa ndio mwisho kwani ukisha jipima sio utaombwa uende kwenye kituo cha kutoa huduma za afya ili uweze kuthibitisha kama majibu uliyopata ni sahihi ama la
Hata hivyo, amesema yamepelekwa bungeni marekebisho hayo ya sheria ili watu waweze kujipima wenyewe lakini pia sheria ya ukimwi inasema mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 18 hawezi kwenda kupima ukimwi bila ridhaa ya wazazi.
“Watoto wetu siku hizi ni watundu pia tumepeleka mapendekezo bungeni. Vijana wa miaka 16 na 17 hawezi kupima mpaka mama au mzazi aandike apime lakini tumeona watoto wanaendelea wana access na mitandao tumepeleka pia bungeni naamini ijumaa wabunge watapitisha mapendekezo yetu tumeshusha mpaka miaka 15 kwenda kupimwa kwenye vituo,” amesema.
Pia,ameongeza kuwa, serikali imeendelea kuwatumia wasanii katika shughuli mbalimbali za kijamii japo kuwa siyo katika kiwango kinachotakiwa ingawa wasanii wana ushawishi mkubwa wa kufikisha ujumbe kirahisi na kwa haraka kwa vijana na mashabiki wao.
“lengo kubwa la kukutana hapa ni kupeana taarifa sahihi ambazo tunaamini zitatusaidia kufikisha ujumbe sahihi kwa wananchi kuhusu virusi vya ukimwi na ukimwi kwa kuanzia njia za kujikinga, huduma za upimaji, tabia hatarishi na hasa huduma za tiba na matunzo,”amesema Mwalimu.
Katika hatua nyingine amesema uelewa wa watanzania kuhusu masuala ya ukimwi katika kila watanzania 100, watanzania 80 wanafahamu kuhusu virusi vya ukimwi na ukimwi.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Benjamini William Mkapa, Dk. Ellen Senkoro amesema taasisi hiyo inatambua vijana kama kundi mojawapo linalokabiliana na vishawishi vingi vinavyosababisha maambukizi ya ukimwi lakini wasanii ni kundi muhimu linaloweza kusaidia kufikia vijana kwa ukaribu zaidi.
"Katika semina hii, tunawanawajengea uwezo wasanii kufikisha ujumbe jinsi inavyotakiwa ukizingatia kuwa ni washawishi wazuri katika kuhakikisha wanapunguza kasi ya maambukizi , unyanyapaa na pia kuhimiza matumizi sahihi ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi (ARV)
Pia,kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba amesema, imekuwa ni desturi kwa wasanii kutangulizwa kufanya jambo hivyo wanaiomba wizara nyingine waige mfano huo kwa kuwa wanafanya kazi kubwa ya kuielimisha jamii.
Naye, Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho, Simon Mwakifamba amesema wasanii wapo tayari kushirikiana na wizara kuhakikisha Sanaa zao zinapeleka ujumbe muafaka.
Mapema, akizungumza katika semina hiyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Yudas Ndungile amesema wizara ya afya imepiga hatua kubwa ya kumaliza na kutoa elimu ya vvu kwa kupitia Sanaa ambapo katika kuhakikisha hilo linafanikia na ujumbe unaifikia jamii sanaa zote zitatumika na wasanii hao watapitishwa kwenye athari za unyanyapaa, kwa jamii juu ya kujikinga na maambukizi, kutumia dawa, jinsi ya kuepuka madawa ya kulevya lakini pia namna ya kuondokana na unyanyapaa
No comments
Post a Comment