Header Ads

Header ADS

Rais Magufuli Afanya Uteuzi Mpya Wa Mdhibiti Na Mkaguzi Wa Hesabu Za Serikali(CAG)

Rais Dkt John Pombe Magufuli leo , Novemba 03, 2019 amemteua Ndugu Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akichukua nafasi ya Prof Mussa Assad.

Prof. Assad aliteuliwa na Rais Mstaafu, Dkt.Jakaya Kikwete wakati wa utawala wake na kuapishwa Novemba 2014

Kabla ya uteuzi wa leo, Kichere alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe na awali alishawahi kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

No comments

Powered by Blogger.