Header Ads

Header ADS

Rais Magufuli amewapiga marufuku Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuacha mara moja kukopa fedha kwenye taasisi za fedha

Rais Magufuli amewapiga marufuku Wakurugenzi  Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuacha  mara moja kukopa fedha kwenye taasisi za fedha kwa madai ya kufanya miradi ya maendeleo.
     Kauli hiyo imetolewa  wilayani Bukombe mkoani Geita wakati akihutubia mkutano wa hadhara, Rais Magufuli amewaagiza iwapo wapo ambao wameshachukua fedha hizo kuzirudisha na kuvunja mikataba waliyoingia.

“Kama kuna mkurugenzi yeyote amekopa fedha azirudishe, mwenye mamlaka ya kukopa kwa niaba ya Serikali ni paymaster general wa Serikali ambaye ni Wizara ya Fedha pekee.” Alisema Magufuli.

“Anayekopa ajiandae kutoka. Naamini Wakurugenzi wamenielewa, nimepita Kahama Mkurugenzi ananiambia anataka kukopa kutoka TIB (Benki ya Uwekezaji Tanzania) kwa ajili ya kujenga stendi, haiwezekani fedha za wananchi kuchezewa, ovyo”  alisema Rais Magufuli




No comments

Powered by Blogger.