Header Ads

Header ADS

RC Chalamila aagiza mawakala mashine za EFD kukamatwa

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya nchini Tanzania, Albert Chalamila ameagiza mawakala wa mashine za kutoa risiti za kielektroniki (EFD)  kukamatwa na kuwekwa ndani kutokana na kutohudhuria mkutano wa wafanyabiashara soko la Sido, jijini Mbeya.
      Mkuu wa Mkoa wa Mbeya nchini Tanzania, Albert
      Ametoa hayo leo katika Mkutano wake na Wafanyabiashara wa Soko kwaajili ya kusikiliza kero zao.
  ''RPC[Kamanda wa Polisi Mkoa] Watafuteni leo Jumamosi wapumzike mahali tutakutana nao Jumatatu ,haiwezekani huu ni upuuzi tunawahitaji wao hawapo hata sisi tumeacha usingizi '' Alisema Chalamila 
              Kutokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Mbeya [TRA] Jijini Mbeya kuna Mawakala wanne kwa sasa ambao walitakiwa kuhudhulia Mkutano huo.

No comments

Powered by Blogger.