Header Ads

Header ADS

Serikali imeagiza mashamba 24 kilosa kupeleka Ilani ya kufutwa.

   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameagiza mashamba 24 yaliyopo katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kupelekewa ilani ya kufutwa kutokana na kutoendelezwa na hivyo kukosa sifa ya kumilikiwa na wamiliki wa hayo mashamba.                                                                     Lukuvi alitoa agizo hilo wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro alipozungumza na uongozi wa wilaya ya Kilosa na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya hiyo akiwa katika muendelezo wa ziara ya kutatua migogoro ya ardhi katika mkoa wa Morogoro.


  Pia Waziri Lukuvi alisema, wilaya ya Kilosa haina kumbukumbu za mashamba jambo lilosababisha wizara yake kuamua kufanya upekeuzi maalum wa mashamba yote katika wilaya hiyo na kubaini mashamba 24 yasiyoendelezwa tofauti na mashamba 48 yaliyopendekezwa kufutwa awali.
   Aidha,Kufuatia agizo hilo la Lukuvi, sasa wilaya ya Kilosa itakuwa na mashamba 72 yanayotakiwa kufutwa baada ya mashamba 48 ya awali kupendekezwa kufutwa kutokana na kutoendelezwa.
  "Maafisa Ardhi  wa Wilaya ya Kilosa mfanye upekuzi wa mashama yote yasiyoendelezwa bila upendeleo wala kumuangalia mtu usoni na wala msitishwe na mtu yoyote kwa cheo chake au utajiri wakati wa kufanya kazi hiyo’’  Lukuvi ameeleza.
  Hata hivyo,Waziri Lukuvi alisema kuwa lengo la serikali kufuta mashamba yasiyoendelezwa ni kuwafikiria wananchi wanyonge wasiokuwa na ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo na kubainisha kuwa mashamba yatakatayofutwa yatagawiwa kwa wananchi na mengine yatatumika kama ardhi ya akiba itakayotumika kwa shughuli za uwekezaji.
Pia, Lukuvi amekemea tabia ya baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kilosa kuuza ama kukodisha mashamba wanayopatiwa na serikali na kusisitiza kuwa katika kukomesha tabia hiyo Wizara yake inaangalia namna ya kugawa mashamba yaliyofutwa  kwa vikundi na kwa wale watakaopatiwa hawataruhusiwa kuuza na kuwataka Maafisa Ardhi kutofanya uhamisho wa shamba kwa yule aliyepatiwa .
"Mkuu wa Wilaya komesha tabia ya udalali wa mashamba unaofanywa na baadhi ya wananchi wa Kilosa na yale mashamba yanayogawiwa kwa wananchi yatumike kwa shughuli zilizokusudiwa’’  Lukuvi alieleza.

No comments

Powered by Blogger.