Header Ads

Header ADS

Serikali yateua Wajumbe wa Bodi ya TANESCO.

   Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amefanya uteuzi wa wajumbe nane wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Alitangaza uteuzi huo jana, Novemba 13, 2019 jijini Dodoma mbele ya waandishi wa habari, viongozi wa Wizara na wa TANESCO.
 Hata hivyo, Waziri huyo alisema kuwa Novemba 9 mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, alimteua Dkt. Alexander Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO kwa kipindi cha pili baada ya kumaliza awamu ya kwanza.

  “Kufuatia uteuzi aliofanya Mheshimiwa Rais, na kwakuwa Wajumbe waliokuwepo muda wao umemalizika Mei 29, mwaka huu, nimewateua Wajumbe hao kwa mamlaka niliyonayo, kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Novemba 13, 2019 hadi Novemba 12, 2022.”

   Aidha,Aliwataja Wajumbe aliowateua kuwa ni Balozi Dkt. James Nzagi ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi hiyo kwa kipindi kilichopita, Dkt John Kihamba ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE), Dkt Lugano Wilson, Mkurugenzi wa TIRDO na John Kulwa, Mkuu wa Idara ya Ukaguzi Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba Muhimbili (MUHAS).
   Hata hivyo, Wengine ni Denis Munumbu, kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), Dkt. Gemma Modu, Mkurugenzi wa  Baraza la Taifa la Vyuo vya Ufundi (NACTE), Mathew Kirama, Mkurugenzi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Dkt Gilay Shamika aliyekuwa Mjumbe wa Bodi iliyopita ya TANESCO.
  Pia, Waziri huyo amemtaka Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi hiyo kufanya kazi kwa nguvu, kasi na ari mpya na kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ili shirika hilo liendelee kufanya kazi vizuri zaidi.
   Aidha, alitoa maelekezo kwa Bodi kuendelea kusimamia shirika hilo kwa weledi na nidhamu, liendelee kufanya kazi vizuri kwa kuwahudumia watanzania wote kwa weledi. “Ni matumaini yetu kwa uzoefu mkubwa mlionao mtaweza kuondoa kero za usambazaji umeme kwakuwa nInyi ndiyo wasimamizi wakuu wa masuala ya nishati nchini.” Dkt Kalemani alisema uteuzi wa Wajumbe hao umeanza rasmi Novemba 13, 2019.

No comments

Powered by Blogger.