Header Ads

Header ADS

TAKUKURU Mkoani Arusha inamshikilia muweka hazina wa kikundi cha ujasiriamali kwa tuhuma za kuiba Tsh millioni 39.

   Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Arusha inamshikilia Muweka hazina wa kikundi cha ujasiriamali cha Imani kwa tuhuma za kuiba Tsh.Million 39 za Wanakikundi na kudai zimeyeyuka kwenye kibubu kwa imani za kishirikina.
   Wiki iliyopita, tamu ya kugawana faida katika kikundi cha ujasiriamali cha Imani Mkoani Arusha iliingia doa baada ya baadhi yao kuzimia ghafla ukumbini kutokana na taarifa ya upotevu wa zaidi ya milioni 39 zilizodaiwa kuyeyuka kwa njia ya kishirikina.
     Hata hivyo,fedha hizo zinadaiwa kuyeyuka ndani ya sanduku la fedha nyumbani kwa muweka hazina wa kikundi hicho chenye wanachama 20.
   Pia,Mmoja wa wanakikundi, Grece Magala alisema kikundi chao chenye miaka mitano tangu kuanzishwa hawajawahi kugawana faida yoyote hadi siku hiyo walipokaa na kukubaliana kugawana faida iliyopo.
  Aidha,baada ya mkasa huo kutokea wanachama hao walikesha wakilia nyumbami kwa Muweka hazina huyo Halima Mwidadi Mkazi wa Osunyai Arusha.
Wengine waliokamatwa na TAKUKURU ni Katibu wa Kikundi Deogratius Seif na Mwenyekiti wake Aisha Saidi ambao walikamatwa jana na kuachiwa kwa dhamana huku Muweka hazina akiendelea kusota Mahabusu kwa sababu za kiupelelezi.

No comments

Powered by Blogger.