Header Ads

Header ADS

TCAA yatakiwa kuongeza ulinzi ili kuepuka ugonjwa ya Ebola


    Wito umetolewa kwa Mamlaka za viwanja vya ndege vilivyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza juhudi kuhakikisha wagonjwa wa Ebola kuingia na kuchangamana na jamii.
   Akizungumza katika mkutano wa kamati ya uwezeshaji usafiri wa anga Afrika Mashariki kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Vallery Chamlungu amesema moja hofu iliyopo ni uwapo wa ugonjwa huo nchi jirani ya Kongo
  
 "Tunahitaji kuweka vifaa vya kisasa na kutoa mafunzo kwa wataalamu wetu na kupambana na Ebola, " alisema Chamlungu. 
  Amesema anaiomba wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na Watoto kushirikiana na mamlaka za viwanja vya ndege kuweka vifaa hiyo. 
  "Ni habari njema kusikia usafiri wa Anga unawezesha kusafirisha abiria na mizigo haraka lakini ni habari mbaya kusikia usafiri wa anga unakuwa chanzo cha kusambaza magonjwa ya kuambukiza, " alisema Chamlungu.
  Pia,ameongeza kwa kusema kuwa, pamoja na kuwapo kwa timu Mahiri ya kupambana na Ebola kwa nchi za Afrika Mashariki lakini  kunahitajika nguvu zaidi ya kuzuia kuingia kwa ugonjwa huo katika nchi zetu.
  Aidha,ameeleza  changamoto kubwa inayoikabili sekta ya usafiri wa anga Duniani kote ni uhaba wa wataalamu wa masuala ya Anga ikiwamo Marubani na wahandisi wa ndege.  
  "Tunahitaji kutoa mafunzo kwa vijana wengi zaidi watakaoweza kukidhi mahitaji yetu pia kwa hapa nchini tumeanzisha mfuko wa mafunzo ambayo TCAA inasimamia, " amesema Chamlungu. 
  Naye Mkurugenzi wa Udhibiti naUchumi wa TCAA, Daniel Malanga alizitaka mamlaka za viwanja vya ndege kutengeneza vyanzo mbadala vya mapato ili kupunguza gharama za utuaji na uegeshaji wa ndege. 
  Hata  hivyo,amesema kuwa ni Vyema kuongeza shughuli nyingine za uchumi katika viwanja vya ndege ambazo zitasaidia kuongeza kipato.
   "Mkutano huu tutajadili namna ya kuongeza mapato katika viwanja vyetu vya ndege ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hotel, maengesho ya magari supermarket," amesema Malanga. 
   Pia, ameongeza kwa kusema watajadili wizi ambao unazikabili viwanja vya duniani hivyo kutasaidia kuongeza idadi watumiaji wa usafiri wa anga. Ameongeza kuwa wanaandaa mango wa kushirikiana na sekta ya kilimo kutafuta soko la mazao yanayoharika haraka waweze kutumia usafiri wa anga kufikia soko.

No comments

Powered by Blogger.