Header Ads

Header ADS

Uongozi Wa Simba Waomba Radhi Kwa Mashabiki

  UONGOZI wa Simba umewaomba radhi mashabiki wake kwa kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui uliochezwa kwenye uwanja wa Kambarage.


Hata hivyo Simba ambayo kwa sasa imecheza mechi saba ilicheza mechi sita bila kupoteza kwenye ligi.

Aidha Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa haina maana ya kufungwa mchezo mmoja wataendelea kufungwa haiwezekani ni jambo la kuketi chini na kupanga mikakakati upya.

"Kupoteza kwetu haina maana kwamba tutaendelea kufungwa ni sehemu ya mpira na tuliyoyapata ni matokeo tumeyapokea.

"Kwa sasa tunachokifanya ni kuendelea kujipanga zaidi kwa ajili ya mechi zetu zinazofuata kwani ligi bado inaendelea,, kikubwa mashabiki watupe sapoti," amesema.

No comments

Powered by Blogger.