Header Ads

Header ADS

Vyama 11 visivyo na uwakilishi Bungeni vyatangaza kushiriki Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 24

   Vyama 11 vya upinzani visivyo na uwakilishi Bungeni vyatangaza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika novemba 24 mwaka huu  vikieleza kuwa ''Anayesusa Chakula ameshiba''.
  Vimetangaza uamuzi huo leo Ijumaa Novemba 8 jijini Dar es salaam siku moja baada ya CHADEMA kujitoa kutoshiriki uchaguzi huo kutokana na Figisufigisu kaika uchukuaji na urejeshaji wa fomu za ugombea na uteuzi wa wagombea.

Vyama hivyo ni DP, NRA, AFP, Demokrasia Makini, UDP, ADC, Ada- Tadea, Sauti ya Umma (Sau), TLP, CCK na UMB

Vimesema vitashiriki vikiamini Wizara ya Tamisemi inayosimamia uchaguzi huo itatenda haki kwa kuwarejesha wagombea wake walioenguliwa kushiriki uchaguzi huo.

“Tunaamini watarudishwa kwa sababu wamekidhi matakwa. Tunataka tushindane kwa hoja na sera kwenye mikutano ya hadhara,” amesema katibu mkuu wa DP, Abdul Mluya kwa niaba ya viongozi wa vyama hivyo.

Amesema, “tutaendelea na uchaguzi kwa sababu siku zote anayesusa chakula ameshiba. Hatuwezi kususia uchaguzi kwa sababu ni mtaji wa kujiimarisha hasa kwa vyama hivi ambavyo havina diwani wala wabunge tofauti na Chadema.”

No comments

Powered by Blogger.