Waarabu Misri waing'oa Yanga Rasmi kombe la shirikisho.
Kikosi cha Yanga jana kimeshindwa kufurukuta mbele ya wapinzani wake Pyramids kwenye mchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho uliochezwa nchini Misri.
Yanga SC waliingia katika uwanja wa 30 June kurudiana na Pyramids wakiwa nyuma kwa magoli 2-1, magoli ambayo yalifungwa katika mchezo wa kwanza jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, hivyo walitakiwa kuifunga Pyramids FC mabao 2-0 ili kupenya mbele hatua ya makundi

Kufunga magoli mawili bila kuruhusu kufungwa haikuwa kitu rahisi kwa Yanga, hivyo walijikuta wakimaliza mchezo huo kwa kupoteza kwa kufungwa kwa magoli 3-0 .
Magoli ya Pyramids FC yalifungwa na Traory dakika ya 27, Farouk 79 na El Said dakika za nyongeza.

Matokeo hayo yanaitoa Yanga kwenye michuano ya kimataifa ambapo Pyramids inafuzu hatua ya makundi kwa juma ya mabao 5-1.
Kwa maana hiyo Tanzania sasa msimu wa 2019/20 haina mwakilishi yoyote wa kimataifa katika michuano hiyo.

No comments
Post a Comment