Header Ads

Header ADS

Jafo aagiza Mweka Hazina na Ofisa Utumishi kukamatwa.

           Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo amemuagiza katibu wake mkuu kuwaondoa kazini Ofisa utumishi wa manispaa ya Shinyanga Magedi Magezi pamoja na Mweka hazina Paschal Makoye, wafanyiwe mabadiliko na kuwapeleka sehemu nyingine wakafanye kazi.
        Jafo ametoa agizo hilo leo Desemba 7,2019 wakati akipokea taarifa ya mkoa wa Shinyanga, kwa mkuu wa mkoa huo Zainab Telack, alipowasili mkoani humo kwa ajili ya kufanya ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Amesema hajaridhishwa na utendaji kazi wa watumishi katika manispaa ya Shinyanga, ambapo kuna makundi na hakuna umoja wa kufanya kazi kwani  kila mtumishi ana sauti kama utawala wa kambale, na kubainisha atafanya mabadiliko ya watumishi kwenye idara mbalimbali ambao hawafanyi kazi vizuri.
      Pia amesema kuwa kutokana na kuwepo na utendaji kazi mbovu katika manispaa ya Shinyanga, amemuagiza katibu wake mkuu, afanye mabadiliko ya kuwaondoa kazini Ofisa utumishi pamoja na Mweka hazina, na kupelekwa sehemu zingine wakafanye kazi , ili kuondoa makundi na kushindwa kufanya kazi ya Serikali vizuri.

“Mkuu wa mkoa kwanza nakupongeza kwa kazi nzuri ambayo unayoifanya, lakini kwenye manispaa yako ya Shinyanga siridhishwi na utendaji kazi wa watumishi kuna tabia ya makundi makundi, hivyo na muagiza katibu mkuu wagu afanye mabadiliko ya kumuondoa Ofisa utumishi pamoja na Mweka hazina,”amesema Jafo.
      “Hatuwezi kuwa na watumishi kila mtu ni Kambale, tunafanya madiliko haya ili kazi ifanyike tuwe na Team work na siyo makundi, pia tutaendelea kufanya mabadiliko hayo kwenye halmashauri zote nchini na jukumu langu mimi ni kumsaidia Rais John Magufuli kuzinyoosha halmashauri,”ameongeza.

Katika hatua nyingine amepongeza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa hatua nzuri ilipofikia, na kubainisha majengo yake yamejengwa kwa kiwango kinachotakiwa, huku akisema Rais John Magufuli wamewaongeza fedha nyingine Shilingi Milioni 500 ili kuongeza majengo mengine.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, akisoma taarifa ya mkoa huo, amesema Serikali ilitoa kiasi cha Shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya kujengwa hospitali mbili za wilaya mkoani humo, ikiwamo hiyo ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambayo imetumia kiasi cha Bilioni 1.5 na imekamilika kwa asilimia 90.

No comments

Powered by Blogger.