Prof. Mkenda ameyasema hayo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 1.2 bilioni kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Kwa Hifadhi nyingine zilizoko chini ya mradi wa REGROW.
Amesisitiza kuwa, ni vizuri kila mmoja kwa nafasi yake akaona umuhimu wa kushiriki kuitangaza nchi kupitia utajiri wa rasilimali iliyojaliwa kuwa nayo jambo ambalo litakuwa na mchango katika ukuaji wa sekta ya utalii na uchumi kwa ujumla.
Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na Mahema, Vifaa vya kukusanyia taarifa (camera, GPS), sare, magodoro buti, vifaa maalumu vya kufanyia doria usiku na vinginevyo vimenunuliwa kupitia mradi wa REGROW.
Awali, Mratibu wa Mradi wa REGROW Saanya Aenea amesema serikali kupitia mradi huo imedhamiria kumaliza changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikabili hifadhi katika ukanda wa kusini mwa nchi na hasa eneo la miundombinu.
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha inapatikana kwa sehemu kubwa mkoani Iringa na ni ya pili kwa ukubwa ikiwa na kilomita za mraba zaidi ya elfu 20.
No comments
Post a Comment