Mfumuko wa bei wa Taifa waongezeka
Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi oktoba 2019.
Hayo yamebainishwa na kaimu mkurugenzi sensa ya watu na takwimu za jamii ofisi ya taifa ya takwimu, Ruth Davison Minja ambapo amesema kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2019.
Aidha,mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 5.1 kwa mwaka ulioishia mwezi oktoba 2019.
Vilevile, Bi.Ruth amesema hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za afrika mashariki Kenya na Uganda umeonekana Kuongezeka ambapo Nchini Kenya Umeongezeka kwa asilimia 5.56 kutoka asilimia 4.95 huku Uganda ukiongezeka kwa asilimia 3.0 kutoka asilimia 2.5.
Ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa sheria ya takwimu kwa mwaka 2015 pamoja na mapitio yake ya mwaka 2018 kwa mujibu wa sheria hiyo, NBS imepewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa taarifa za kitakwimu nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za mfumuko wa bei kwa ajili ya matumizi ya serikali na wadau wa takwimu.
No comments
Post a Comment