Header Ads

Header ADS

Moto waua Wafanya kazi zaidi ya 40 India

       Moto mkubwa ulioteketeza kiwanda cha begi katika mji mkuu wa India Delhi, umewaua wafanyikazi 43, maafisa wanasema.
Moto huo ulizuka katika jumba la ghorofa nne katika eneo la kale la makaazi lenye msongamano Jumapili asubuhi.
Karibu watu 100 walikuwa wamelala ndani ya kiwanda hicho, ambacho hutengeneza mabegi ya shule, wakati moto ulipoanza. Zaidi ya watu 60 wameokolewa.


Waziri mkuu Narendra Modi aetaja tukio hilo kuwa la "kusikitisha" na kutuma risala zake za rambirambi kwa walioathiriwa.

Moto huo ilianza katika vyumba vya chini vya jengo hilo na kusambaa hadi ghurofa ya tatu ambapo wafanyikazi walikuwa wanalala.

"Niliamshw ana kelele za watu wanaoomba msaada," alisema Ronak Khan, mwenye umri wa miaka 17-anaeishi nyumba jirani.

"Niliona watu wamekwama ndani. Tuliwashauri wapande juu wa paa la nyumba ili tuweze kuwasaidia lakini hawakuweza kufanya hivyo."

Eneo ambalo kiwanda hicho kipo ni karibu na - siko la Azad - ambako njia ni nyembamba, hali iliyowapa wazima moto changamoto ya kupafikia.

Waokoaji walilazimika kuwabeba majeruhi mabegani mmoja baada ya mwingine, alisema mwandishi wa BBC Idhaa ya Kihindi, Dilnawaz Pasha kutoka eneo la tukio.

Haijabainika ni nini kilichosababisha moto huo lakini agizo la uchunguzi kufanywa limetolewa.

Mmoja wa mashuhuda ametaja hitilafu za umeme kuwa chanzo chake.

Watu kadhaa waliojeruhiwa katika mkasa huo kwa sasa wanapoke amatibabu katika hospitali tofauti mjini humo.

Jamaa za waathiriwa wamekuwa wakitafuta taarifa kuhusu hatma ya wapendwa wao. Mtu mmoja ameliambia shirika la PTI nchini India kuwa ndugu yake alikuwa ndani ya jengo hilo.

"Nilipigiwa simu na rafikia yake kunifahamisha kuwa amejeruhiwa katika mkasa huo. Sina habari amepelekwa hospitali gani," alisema.

Miji ya India imekuwa ikikabiliwa na visa vibaya vya moto, huku mpangilio mbaya wa makazi na kuzembea kwa maafisa katika suala la kuzingatia kanuni za usalamakama chanzo kuu cha mkasa huo.

No comments

Powered by Blogger.