Header Ads

Header ADS

Naibu Waziri Wa Elimu Ole Nasha Awataka Wakuu Wa Shule Kushawishi Wanafunzi Kuchangamkia Mashindano Ya Insha Ili Kukuza Uwezo Wa Lugha.

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe,William Tate  Ole Nasha amewaasa Wakuu wa Shule kote nchini kuendelea kuwashawishi wanafunzi kuchangamkia Fursa za Mashindano ya  uandishi wa insha ili kukuza uwezo wa Lugha na mada za masomo mbalimbali. yamesemwa hayo jijini Dodoma katika hafla ya kutunukia vyeti kwa washindi wa kitaifa  wa uwandishi wa insha ya jumuiya ya maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) na jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).


  Naibu waziri ,Nasha amesema Mashindano ya  uandishi wa Insha yanaongeza Maarifa kwa ujumla  na kusaidia wanafunzi siku za usoni kunufaika na mtangamano wa Jumuiya za SADC na EAC katika kujipima na kujilinganisha kitaaluma na wanafunzi wa nchi nyingine ambapo pia mashindano hayo hutoa ari,hamasa na msukumo  kwa wanafunzi kupenda kushiriki mashindano mbalimbali yajayo katika ngazi za juu zaidi.Aidha,Mhe.Nasha ametoa wito kwa wakuu wa shule zote  nchini kusimamia kwa makini mchakato wa Mashindano hayo na kuagiza kila mkuu wa shule kuteua mratibu  atakayefanya kazi ya kusimamia wanafunzi  ili kuzingatia na kufuata taratibu zote za uandishi wa insha.Aidha,Mhe.Nasha ametoa wito kwa wakuu wa shule zote  nchini kusimamia kwa makini mchakato wa Mashindano hayo na kuagiza kila mkuu wa shule kuteua mratibu  atakayefanya kazi ya kusimamia wanafunzi  ili kuzingatia na kufuata taratibu zote za uandishi wa insha.
 
Pia ,Naibu Waziri Nasha amesema Uandishi wa insha unawapa uwezo wanafunzi hamasa katika kutafiti na kupata taarifa na uelewa  zaidi kuhusu mada inayoshindaniwa na kuongeza utambuzi zaidi kuhusu maendeleo ya Jumuiya za SADC na EAC ambapo tafiti hizo husaidia kupambanua masuala katika sekta mbalimbali .

"Ili tupate washindi wengi katika mashindano haya ni lazima wakuu wa shule za Sekondari wahakikishe wanawahamasisha Sana wanafunzi wengi kushiriki katika mashindano hayo, kwa sababu yanawaongezea fulsa washiriki na kuwasaidia kujiamini Sana"

"Mashindano haya yanawasaidia wanafunzi wetu kuwajengea uwezo wa uandishi, udadisi na kuwa wepesi kufanya tafiti,pia mashindano haya yanasaidia kuwajengea uzalendo pindi wanapokuwa wanawakilisha taifa" amesema Ole Nasha.

Amesema maada iliyoshindaniwa katika shindano hilo kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa "ni kwa namna gani aina mbalimbali za Utamaduni wa watu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaweza kutumiwa kuimarisha utengamano wa kikanda, ukuaji wa uchumi na utalii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki".

Kwa upande wa Jumuiya ya SADC ilihusu "ni kwa namna gani mipango inayolenga vijana inachangia katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika ukanda wa SADC"? mada zote mbili zimekuwa Chachu ya mipango ya maendeleo kwa vijana wa Nchi wanachama.
 
Naye mratibu wa tukio hilo na la uandishi wa insha Sylvia Chinguwile, amesema maada za zinazoshindaniwa huzingatia makubaliano ya wakuu wa Nchi na baadaye Nchi wanachama kuwajibika kutangaza na kubainisha vigezo vya washiriki.
 
Amesema baada ya kupita katika michakato huo huwasilishwa wizarani na kuteuliwa insha bora katika ngazi ya shule na kusahihishwa na jopo la wataalamu na zile za EAC husimamiwa na balaza la mitihani, na insha tatu bora za SADC hupelekwa Botswana ili kuidhinishwa na mataifa Nchi wanachama, wakati insha tano bora huwasilishwa Arusha Makao makuu ya Jumuiya kushindanishwa na Mataifa mengine.
 
Amesema kwa upande wa EAC mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza ni Vanessa Lema, kutoka Longido Sekondari kidato Cha sita, wakati wa pili ni Thomas Kalisti, Kibasila Sekondari Dar as saalam kidato Cha Tatu, huku kwa ujumla wake Wakiwa 13.
 
Kaimu Kamishna wa Elimu hapa nchini Mwalimu Augusta Lupokela, ameipongeza Wizara ya elimu kwa kuweza kuwasimamia mwanzo hadi mwisho wa mashindano hayo amesema kupitia mashindano hayo wameweza kujipambanua kuwa bado elimu yetu ipo katika Hali nzuri ukilinganisha wanavyoiongelea watu wengine.
 
Mmoja wa wanafunzi ambaye alifanya vizuri katika uandishi wa Insha kwa maada zote Julieth Mpuya, kutoka Kilangalanga Sekondari kidato Cha kwanza, amesema kilichompelekea kufanya vizuri ni ujasiri, kujituma kufuatilia maada na kuamini kuwa anaweza na hatimaye kufanya vizuri.
 
Katika Mashindano hayo Mshindi wa Kwanza kwenye Jumuiya  SADC amejishindia dola za Kimarekani mia tano na upande wa Jumuiya ya  EAC akijinyakulia  dola za Marekani Mia tatu.

No comments

Powered by Blogger.