Soko la ajira halikidhi Idadi ya Wahitimu Nchini
Serikali imesema kuwa Soko la ajira rasmi nchini ni dogo sana na hivyo halikidhi mahitaji ya wahudumu wote kwa hali hiyo wahitimu hao wanatakiwa kukabiliana na changamoto ya Soko hilo kwa kuelekeza mawazo yao kwenye kujiajiri badala ya kuajiriwa.Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shaban wakati akimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango katika mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara yaliyofanyika katika Viwanja vya Kampasi jijini Dar es Salaam.Amesema kuwa kwa wale wahitimu wenye ajira msingi mkuu wa mafanikio ni kufanya kazi kwa kuzingatia sera,Sheria,Taratibu na Kanunu ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vishawishi au vitendo vya rushwa na ubadhirifu kwa kuwa vina madhara makubwa ya maisha ya mtu Mmoja moja na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla. Shaban amesema elimu inayotolewa na TIA imejikita kwenye fani za Uhasibu ikiwemo Uhasibu wa Fedha za Umma, Ununuzi na Ugavi,Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa Rasilmali Watu pamoja na Masoko hivyo fani hiyo ni nguzo muhimu katika kuendesha Uchumi wa Taifa hususani katika kusimamia mapato na matumizi ya Fedha za Umma.Naibu Katibu Mkuu huyo amesema sera yetu kwa sasa ni uchumi wa viwanda hivyo umahiri wa wataalam wanaozalishwa unatakiwa kuonekana ili kufanikisha azima ya serikali ya Tanzania ya Viwanda.Shaban amekazia katika kukabiliana na changamoto za Usimamizi wa Mapato na matumizi ya Fedha za Umma,mahitaji ya Soko ,Ushindani na Utandawazi hamna budi Taasisi ya Uhasibu nchini (TIA) Kuendesha Shughuli kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa ya kupeana na kubadilishana taarifa kwani watalaam wanaohitajika ni wenye weledi,maarifa na umahiri wa kutatua za changamoto na si kuongeza changamoto kwa Wananchi katika kupata huduma.Amesema kuwa TIA izingatie umakini wa suala la umahiri katika mitaala ili kuweza kuwa na wataalam wenye uwezo wa kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa Kipato cha kati kabla ya 2025.Mwenyikiti wa Bodi ya Wizara ya Fedha na Mipango Wakili Said Chiguma amesema kuwa waajiri wa sekta ya Umma na binafsi wamekuwa wakiona mafanikio kwa wahitimu wa TIA kuwa na sifa zilizotukuka katika kufanya kazi licha ya kuwapo kwa Vyuo vingi nchini na kufanya Chuo hicho kuendelea kuongeza idadi ya udahili kwa wanafunzi kusoma kwa kila mwaka.Amesema Taasisi ina wanafunzi zaidi ya 19,000 katika Kampasi Sita za Kimkakati.Nae Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Luciana Hembe amesema kuwa wahitimu katika Chuo hicho wameweza kjfundishwa ujasiriamali ili kuweza kujiajiri katika kukabiliana na changamoto ya ajira nchini.Amesema Chuo kumekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakiksha wahitimu wanajiajiri katika maeneo Mbalimbali ya kuweza kukidhi mahitaji yao pamoja Taifa kunufaika na maarifa yao ya kujiajiri.Aidha amesema kuwa Baadhi wahitimu katika Taasisi hiyo wa miaka iliyopita wameweza kuanzisha Kampuni mbalimbali ambazo ziko katika Ushindani wa kibiashara na Kampuni zingine.Amesema wahitimu wa mwaka 2019 nao watumie ujuzi na maarifa yao katika kufungua milango ya ajira ya kujiajiri ili wasitumie muda mwingi wa kusubiri ajira katika sekta ya Umma na binafsi.
x
No comments
Post a Comment