Header Ads

Header ADS

Elimu ya kujikinga na Ugonjwa yatolewa Mkoni Songwe.

    Ili kujikinga na Mlipuko wa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola Wizara ya Afya   Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imetoa mafunzo kwa watu 442 mkoani Songwe namna ya kupambana na kujikinga na ugonjwa kwa kuwatambua watu wenye dalili za ugonjwa wanaongia nchini kutoka nchi  jirani.
   Afisa Progamu kitengo cha Elimu ya afya kwa umma Idara ya Afya , Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Tumaini Haonga alisema kuwa wamebaini kuwa mikoa tisa (9) nchini ipo hatarini kupata ugonjwa wa ebola kutokana na kuwa mipakani na mingine kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu uliopo kati ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na nchi yetu ya Tanzania.
  
    Alisema mpaka hivi sasa wametoa mafunzo kwa watu 3200 nchi nzima, huku mkoa wa Songwe watu 442 wakiwa tayari wamepata elimu  namna ya kumtambua mtu mwenye ugonjwa wa Ebola namna ya kujikinga na maambukizi pindi ugonjwa huo unapobainika na kufahamu namna ya uenezaji.
  “Mpaka hivi sasa ugonjwa wa Ebola nchini Congo walobainika kupata Ugonjwa huo ni jumla ya watu 3398 , vifo vilivyotokea ni 2235 sawa na asilimia 66, sehemu zilizo athirika zaidi ni Jimbo la Kivu na Ituri kaskazini mwa nchi hiyo kutokana na eneo hilo kukumbwa zaidi na machafuko ya vita" alisema Dkt Tumaini .
    Dkt Tumaini Haonga alisema kuwa wamebaini kuwa mikoa tisa (9) nchini ipo hatarini kupata ugonjwa wa ebola kutokana kuwa mipakani na mingine kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu uliopo kati ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na nchi yetu ya Tanzania.
   Aliongeza kuwa Mkoa wa Songwe upo hatarini kwa halmashauri za mji wa Tunduma, Momba na Mbozi kutokana na kupokea wageni wengi kutoka nchi za kusini mwa Afrika, Kwa kuliona hilio Wizara ya afya imeamua kutoa mafunzo ya namna ya kujikinga na kujua dalili kupitia kwa watalam wa afya na wahudumu ngazi ya jamii, viongozi wa dini, viongozi wa usafirishaji na viongozi wa Tiba asilia lengo likiwa ni kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi.
    "Tumebaini mikoa tisa ya Songwe, kagera , DaresSlaam, Mbeya, Rukwa, Katavi,Mwanza Kagera na Kigoma, hii ni kutokana na kuwa mipakani na mikoa mingine kama Daresslaam na Dodoma  kuwa na mwingiliano mkubwa wa watu wanaotoka mipakani mwanchi" aliongeza Dkt Tumaini.
   Alizitaja dalili kubwa za Ebola kuwa ni  kuonyesha dalili ya homa, mwili kutoka damu sehemu mbalimbali,kutapika, mwili kuchoka , kuharisha damu mfululizo, mafua makali , kutoka machozi  , maumivu ya tumbo na ngozi kuvilia damu.
    Aidha alisema njia kubwa ya kuenea kwa Ebola ni kugusa majimaji ya mwili kutoka kwa mtu mwenye ugonjwa,  mkojo, damu, matapishi, kinyesi, mbegu za kiume pamoja na maziwa ya mama.
    Naye Simon Kadogosa kiongozi kutoka msalaba mwekundu nchini alisema kuwa  mafunzo hayo ya kupambana na mlipuko wa ebola yanatolewa katika makundi matatu ya ambapo ni kwa upande wa viongozi wa Halmashauri ambao huweza kusambaza elimu kwa njia ya mikutano na wananchi , watoa huduma ngazi ya jamii ili kutoa elimu nyumba kwa nyumba kuhusina na ebora na kundi la tatu ni kundi la watu maalumu kama vile machifu na na waganga wa jadi ambao huweza sambaza elimu pia wananchi.
   Alisema mpaka hivi sasa kwa nchi ya Tanzania hakuna mgonjwa yeyote ambaye amebainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa, lakini wanaendelea kutoa elimu ili iweze kusambaa nchi nzima kwa wananchi hasa waishio kwenye mikoa ambayo iko mpakani kujua historia ya ugonjwa, uenezaji na namna ya kujikinga
   .Ezenia Pwele kutoka kata ya Nanyara wilayani Mbozi ni miongoni mwa  waliopata mafunzo alisema wamejifunza namna ambavyo jamii inatakiwa ichukue tahadhari kwa watu wegeni wanaoingia nchini kuhakikisha wanatoa taarifa kwa viongozi na kama ana dalili kutoa taarifa bila kwa wataalam wa afya bila ya kumgusa mgonjwa.
    naye Oliver Nzowa mhudumu afya ngazi ya jamii kata ya Hasanga alisema wamejifunza namna ya kutoa elimu kwa wananchi namna ugonjwa unavoenea na dalili za ugonjwa huo ambapo kama mtaalam wa afya ngazi ya jamii atakuwa balozi kuelimisha.
   Kwa upande wake afisa afya Mkoa Songwe George Mgallah alisema  kwa kuwa mkoa wa Songwe umebainika kuwa na hatari ya kuweza kupata maambukizi ya Ebola kutokana na kuwa lango kuu la nchi za kusini mwa Afrika wamejipanga kuendelea kutoa elimu ndani ya mkoa hasa kwa Halmashauri za Tunduma , Momba na Mbozi  kwa kutumia  watalaamu wa afya ngazi ya wilaya ngazi ya jamii na watu maarufu kama vile viongozi wa mila na tiba asilia
   Aidha alisema wanaanda vipeperushi mbalimbali na ambavyo vitakuwa vinasambazwa katika sehemu mbali mbali zenye mikusanyiko na mashuleni ndani ya mkoa wa Songwe.

No comments

Powered by Blogger.