Kampuni ya Barrick Gold Yaahidi Kujifunza Kutokana Na Makosa Yaliyofanyika Tanzania
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Barrick Gold, Dk Mark Bristow amesema kampuni hiyo itajifunza kwa makosa iliyoyafanya nchini Tanzania miaka 10 iliyopita.
Dk Bristow ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Januari 24, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kamati ya madini ya Barrick.
Amesema tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani kumekuwa na safari ndefu ya majadiliano kati ya kampuni hiyo na Serikali yaliyowezesha kugawana mapato sawa.
“Sisi wawekezaji tunapokuja kwenye nchi kama hii tuna jukumu kubwa la kuchimba rasilimali ya Taifa si kwa faida yetu tu bali kwa faida pia ya Taifa na wadau wengine. Wadau hao siyo tu wanahisa, bali wananchi ndiyo maana ni wajibu wetu kulipa kodi.”
“Vilevile siyo tu kwa Watanzania wa sasa bali pia vizazi vijavyo vina haki ya kupata mgawo. Kuna jamii zinazozunguka migodi, lazima zishiriki shughuli za uchumi,” amesema.
Baada ya mgogoro uliodumu tangu mwaka 2017, Kampuni ya Barrick na Serikali ziliunda kampuni ya Twiga itakayosimamia migodi mitatu iliyokuwa chini ya kampuni ya Acacia.
No comments
Post a Comment