Header Ads

Header ADS

Kiongozi wa kidini wa Iranametetea majeshi kwa kudungua ndege ya Ukraine.

  .Kiongozi mkuu dini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametetea majeshi ya nchi yake baada ya kukiri kuwa ilidungua ndege ya abiria ya Ukraine kimakosa.
  Amesema kikosi maalum cha majeshi ya ulinzi ya Iran Revolutionary Guard - kilichohusika na mkasa huo kilikuwa - "kinalinda usalama" wa Iran.

Picha ya Ayatollah Ali Khamenei siku ya Ijumaa
    Maandamano ya ndani ya nchi na ukosoaji kutoka mataifa ya kigeni yameiweka Iran mashakani kuhusisna na jinsi inavyoshughulikia tukio hilo. 
   Lakini Ayatollah alitoa tamko hilo wakati wa alipoongoza sala ya Ijumaa mjini Tehran kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012.
   Ametoa wito wa "umoja wa kitaifa" na kusema kuwa "maadui" wa Iran - akiashiria Washington na washirika wake - wanatumia ajali hiyo ya ndege kuzima mauaji ya jenerali Qasem Soleimani.
  "Mamilioni ya raia wa Iran na maelfu ya raia wa Iraq walimuomboleza [Soleimani]," alisema.
   Ndege aina ya Boeing 737-800 ya shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilikuwa inasafiri kuelekea Kyiv kutoka Tehran Januari 8, ilipoanguka muda mfupi baada ya kuanza safari.
   Abiria wote 176 waliokua ndani ya ndege hiyo wengi wao raia wa Iranian na Canada, walifariki.
   Utawala wa pia uko kwenye shinikizo kutokana na kuporomoka kwa uchumi hali iliyosababishwa na vikwazo vya Marekani.
   Ayatollah Khamenei, 80, alihutubia taifa kutoka msikiti wa Mosalla uliopo mji mkuu wa Tehran.
   Mara ya mwisho alifanya hivyo ilikuwa mwaka 2012 wakati wa kumbukizi ya miaka 33 ya mapinduzi ya kiislam katika nchi hiyo.
   Akiwatetea wanajeshi , Ayatollah pia:
  • Alikosoa na kuutaja kuwa wenye "chuki" utawala wa rais wa Marekani Donald Trump
  • Alisema hatua ya Iran kushambulia kwa makombora vituo vya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq ilikuwa"kofi la usoni" kuonesha Marekani kuwa"Mungu anaunga mkono" Iran
  • Alielezea kikosi maalum cha Quds - ambacho Marekani imetambua kama shirika la kigaidi - kuwa "shirika la kibinadamu linalothamini utu"
  • Alitaja mazishi ya Soleimani na hatua ya majeshi ya the Iran kama "mwanzo mpya wa kihistoria"
Siku ya Jumatano, Rais Hassan Rouhani aliomba kuwepo kwa mshikamano wa kitaifa.
  Lakini katika ishara ambazo hujitokeza kwa nadra ndani ya utawala wa Iran, rais Rouhani amelitaka jeshi kuwajibika kwa kutoa maelezo ni kwa vipi waliidungua ndege ya Ukraine.
  Ndege aina ya Boeing 737-800, iliyokuwa ikisafiri kwenda Kyiv ikiwa na abiria wegi waliokuwa wakielekea Canada, iliangukamuda mfupi baada ya kupaa kutoka Tehran, tukio lililogharimu maisha ya watu 176 waliokuwa kwenye ndege.
  Kwa siku tatu mamlaka za Iran zilikana kuhusika na tukio hilo lakini baada ya shinikizo kutoka kwa jumuia ya kimataifa, jeshi lilikiri kuwa ndege hiyo ilishambuliwa kimakosa wankati wa msuguano kati ya Iran na Marekani.
  Saa chache kabla, makombora ya Iran yalilenga kambi mbili za jeshi la anga nchini Iraq zilizokuwa na wanajeshi wa Marekani.
  Shambulio la roketi lilikuwa kisasi baada ya ndege isiyo na rubani ya Marekani kufanya shambulizi Baghdad na kusababisha kifo cha jenerali Qasem Soleimani.
Njia ya ndege

No comments

Powered by Blogger.