Mchungaji Amuua Mkewe Kwa Kisu
Mchungaji wa kanisa moja jijini Mombasa nchini Kenya amemuua mkewe kwa kumchoma kisu wakati wa ibada kanisani kwake kutokana na ugonvi wa kifamilia. Mchungaji huyo aliyetajwa kwa jina la Elisha Misiko wa kanisa la ‘Ground For Jesus’ alitoa kisu ghafla wakati ibada ikiendelea na kumchoma mkewe mgongoni na kichwani hadi kumuua.
Kwa mujibu wa waumini wa kanisa hilo, wakati bado waumini wakiwa na taharuki, mchungaji huyo alijikata koromeo kwa kutumia kisu hicho na akapoteza maisha pia.
Kamanda wa Polisi wa Kisauni, Julius Kiragu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi. Kamanda Kiragu amesema kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita, majira ya saa nne asubuhi.
Ameeleza kuwa baada ya kufanya upekuzi, walimkuta mchungaji huyo akiwa na ujumbe wenye kurasa 17 unaoelezea kusudio la kujiua na mgogoro wa ndoa kati yake na mkewe.Polisi hawakuweka wazi ujumbe huo.
No comments
Post a Comment