Mwanamke tajiri Afrika ''Alivyoipora Nchi yake''.
Isabel dos Santos alipata mikataba ya faida kubwa inayojumuisha ardhi, mafuta, almasi na simu wakati baba yake alipokuwa rais wa Angola, nchi iliyoko kusini mwa Afrika yenye utajiri wa maliasili. Hati hizo zinaonyesha jinsi yeye na mumewe walivyoruhusiwa kununua mali za serikali katika safu ya mikataba mibaya Bi Dos Santos anasema madai dhidi yake ni ya uwongo na kwamba kuna uwindaji wa kisiasa unaofanywa na serikali ya Angola dhidi yake
Binti huyo ambaye ni wa rais wa zamani nchini humo ameifanya Uingereza kuwa nyumbani kwake na anamiliki mali ghali katikati mwa London Tayari yuko chini ya uchunguzi wa jinai nchini Angola kwa ufisadi na mali zake zimezuiliwa. BBC Panorama imepewa idhini juu ya ufikiaji wa hati zaidi ya 700,000 zilizovuja juu ya ufalme wa biashara wa bilionea huyo mwanamke barani Afrika. Mpaka kufikia sasa, Isabel amechunguzwa na mashirika ya habari 37 ikiwa ni pamoja na gazeti la The Guardian na gazeti la Exresso la Ureno. Andrew Feinstein, mkuu wa kituo cha ufisadi, anasema nyaraka zinaonyesha jinsi Bi Dos Santos alivyoinyanyasa nchi yake kwa kuwadhulumu watu wa kawaida wa Angola. "Kila wakati amekuwa akionekana kwenye jarida moja la glossy na mahali pengine ulimwenguni, kila wakati anapofanya sherehe za kukata na shoka huko kusini mwa Ufaransa, anapofanya hivyo ni sawa na ICIJ imezitaja stakabadhi hizo kama Luanda Leaks Moja ya biashara yenye utata iliendeshwa kutoka London kupitia kampuni tanzu ya Angola nchini Uingereza Sonangol. Bi Dos Santos ilikuwa akisimamaia kampuni ya Sonangol mwaka 2016, ambapo alipata ulizi wa rais ambaye ni baba yake Jose Eduardo dos Santos, aliyeiongoza nchi kwa miaka 38. Lakini alipostaafu kama rai s mwezi Septemba mwaka 2017 alikabiliwa na hatari ya kupoteza wadhifa wake, japo aliyemrithi Bw. Jose Eduardo dos Santos alitoka chama chake. Bi Dos Santos alifutwa miezi miwili baadae. Raia wengi wa Angola wameshangazwa na hatua ya rais Joao Lourenço ilivyolenga maslahi ya kibiashara ya familia ya mtangulizi wake. Hati zilizovuja zinaonyesha kuwa wakati anaondoka Sonangol, Bi Dos Santos aliidhinisha $58m ya malipo tata kwa kampuni ya ushauri huko Dubai inayoitwa Matter Business Solutions.
Anasema hana nia ya kifedha kwa jambo lolote, lakini nyaraka zilizovuja zinaonyesha zilisimamiwa na meneja wake wa biashara inayomilikiwa na rafiki.
BBC Panorama inaarifu kuwa Bi Isabel alituma stakabadhi za kudai malipo zaidi ya 50 kwa Sonangol huko London siku ambayo alifukuzwa.
Bi Dos Santos anaonekana kupitisha malipo kwa kampuni ya rafiki yake baada ya kufutwa kazi.
Ingawa kazi fulani ya ushauri ilifanywa na kampuni ya Matter, kuna maelezo kidogo sana juu ya stakabadhi za kuhalalisha bili kubwa kama hizo.
Moja inadai paundi 472,196 kwa gharama zisizojulikana, nyingine dola za 928,517 kwa huduma za kisheria ambazo hazijajulikana.
Malipo yenye utata
Mchezo ulikuwa ukichezeshwa kwa namna hii, malipo mbili tofauti na - kila moja inadai paundi 676,339.97- kwa kazi ile ile, kwa tarehe hiyo hiyo na Bi Dos Santos akawa akisaini zote.
Mawakili wa Matter Business Solutions wanasema kampuni hiyo ilibuniwa kusaidia kuleta mabadiliko katika sekta ya mafuta na kwamba malipo hayo yalikuwa ya kazi ambayo ilikuwa imefanywa na kampuni zingine tanzu ilizokuwa imeipatia kazi.
"Kuhusu malipo yaliyohusiana ni jambo la kawaida kwa makampuni kuongeza gharama katika malipo mengine kwa ujumla. Hii inatokana na gharama inayohusiana na kazi za kuweka pamoja mchakato mzima wa kujiandaa kikazi... Matter inaweza kuwasilisha stakabadhi za kuthibitisha hilo kukadiria gharama zote ilizolipa."
Mawakili wa Bi. Dos Santos wamesema hatua yake kuhusiana na malipo ya kampuni ya Matter ilikuwa halali na kwamba hakuidhinisha malipo yoyote baada ya kufutwa kazi Sonangol.
Walisema: "Malipo yote yaliyohusiana na huduma ilizotoa ilikuwa makubaliano kati ya washirika wawili wa kibiashara, ambayo yalijumuishwa katika mkataba ambao ulifikiwa chini ya ufahamu wa wakurugenzi wa bodi ya usimamizi ya Sonangol."
ICIJ na Panorama pia imepata maelezo kuhusu biasha iliyomfanya Bi Dos Santos kuwa tajiri.
Sehemu kubwa ya mali yake ilikuwa kupitia umiliki wa hisa katika kampuni ya kawi ya Galp ya Ureno, ambayo ilikuwa moja ya makampuni yaliyonunua mafuta kwa kampuni ya mafuta ya Sonangol mwaka 2006.
Stakabadhi zinaonesha kuwa alihitaji kulipa 15% ya bei halisi mwanzoni na kukamilisha fedha zilizosalia ya €63m ($70m) ambayo ilibadilishwa kuwa mkopo wa riba ya chini kutoka Sonangol.
Chini ya mkopo huo wenye mashariti hafifu na ya kuvutia, deni lake kwa watu wa Angola halikuhitaji kulipwa kwa miakakwa miaka kumi na moja.
Umiliki wake katika kampuni ya Galp sasa ni wa thamani ya zaidi ya €750m.
Kampuni ya Bi Dos Santos ilijitolea kulipa deni la Sonangol mwaka 2017.
Ofa ya kulipa deni hili ingelikuwa imekataliwa kwa sababu haikujumuisha riba ya €9m iliyokuwa inadaiwa.
Lakini Bi Dos Santos alikuwa msimamizi wa Sonangol wakati huo na alipokea fedha hizo kama malipo kamili ya deni alililokuwa akidaiwa.
Alifutwa kazi miaka sita baadae na malipo hayo yalirudishwa na usimamizi mpya wa Sonangol.
Bi Dos Santos anasema wazo la kuwekeza katika kampuni ya Galp lilikuwa lake na kwamba kampuni ya Sonangol pia ilifaidika na uwekezaji huo.
"Hakuna makosa yoyote ylaiyotokana na biashara hiyo. Uwekezaji huu ni uwekezaji ambao katika historia umefaidi kampuni ya kitaifda ya mafuta na kandarasi zote zilizoandikwa zilizingatia sheria, kwa hiyo hakuna makosa yaliyofanyiika."
Mawakili wake wanasema ofa ya kulipa deni mwaka 2017 ilijumuisha deni ambalo lililokuwa linadaiwa na Sonangol.
Tawira katika sekta ya almasi noi sawa na ile ya mafuta .
Bi Dos Santos na mume wake, Sindika Dokolo, walitia saini mkataba ulioegemea upande mmoja mwaka 2012 na kampuni ya kitaifa ya almasi ya Angola,Sodiam.
Walitakiwa kuwa washirika wa kibiashara watakaonufaika nusu kwa nusu katika mkataba
wa kibiashara na kampuni ya vito vya thamani ya Uswizi ya De Grisogono.
Lakini uwekezaji huo ulifadhiliwa na kampuni ya serikali. Stakabadhi zinaonesha kuwa miezi 18 baada ya uwekezaji huo, Sodiam ilikuwa imelipa $79m katika ushirikiano huo, huku Bw. Dokolo akiwa amewekeza $4m pekee.
Sodiam pia ilimpatia €5m kwakufanikiwa kuleta biashara hiyo, hii inamaanaisha hakuhitaji kutumia fedha zake kulipia uwekezaji huo.
Bishara ya almasi ndio iliyowamaliza kabisa watu wa Angola.
Stakabadhi zilizofichuliwa zinaonesha jinsi kampuni ya Sodiam ilivyokopa fedha kutoka fedha kutoka kwa benki ya kibinafsi ambayo Bi Dos Santos alikuwa mwanahisa mkuu.
Sodiam italazimika kulipa riba ya 9% na mkopo wa ambao ulioidhinishwa na mamlaka ya rais, ili benki ya Bi Dos Santos isipate hasara.
Bravo da Rosa, afisa mkuu mtendaji mpya wa Sodiam, aliambia Panorama kuwa watu wa Angola hawakupata ha dola moja kutoka kwa uwekezaji huo: "Mwisho wa siku, tutakapomaliza kulipa deni hilo, Sodiam itakuwa imepoteza zaidi $200m."
Rais wa zamani wa Angola pia alimpatia mume wa Bi Dos Santos haki ya kununua almasi ambayo haijasafishwa.
Isabel dos Santos ni nani?
- Binti mkubwa wa Rais wa zamani wa Angola Jose Eduardo dos Santos
- Aliolewa na msanii kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye pia ni mfanyabiashara Sindika Dokolo
- Kwa kiasi kikubwa amesoma nchini Uingereza mahali ambako anaishi mpaka sasa
- Inaarifiwa kuwa Isabel dos Santos ndiye mwanamke tajiri zaidi barani Afrika na kukisiwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni mbili
- Isabel anatajwa kumiliki kampuni za mafuta na simu za rununu na benki, haswa nchini Angola na Ureno.
No comments
Post a Comment