Header Ads

Header ADS

Naibu Waziri wa Afya Dr Ndugulile Ashangazwa Na Uchapa Kazi Wa Wanawake Ludewa.

       Ahimiza wanawake wa mikoa mingine kuiga mfano wa udhubutu wa wanawake hao.
  Aaagiza Halmashauri kuwapatia tenda ndogo katika ujenzi wa barabara na madaraja madogo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amewtaka wanawake na vijana nchini kutumia changamoto zilizopo katika maneo yao kama fursa ya kujiajiri na kuajiri watu wengine.
   Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wilayani  Ludewa mkoani Njombe wakati alipotembeela vikundi kazi vya wanawake na vijana vinavyojishughulisha na kutengeneza barabara na madaraja madogo wilayani humo. 

  Dkt.Ndugulile ameongeza kuwa vijana na wanawake wengi wamekuwa wakilalamika kukosa ajira hasa kwa walimaliza elimu ya juu ila wanawake na vijana wa wilaya ya Ludewa wamedhubutu kuchangamkia fursa ya kutengeneza barabara na madaraja madogo.

“Sijawahi kuona kitu kama hiki tangu nianze ziara zangu katika mikoa na wilaya hongereni mmedhubutu na mkaamua ktuia fursa hii kupatakujiajir ni mwanzo mzuri mtafika mbali" alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Ameogeza kuwa jambo linalofanywa na vikundi hivyo linaendana moja kwa moja na dhana ya Maendeleo ya Jamii  ya wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo katika maneo  yao kwa kuamsha ari yao katika kushiriki shughuli hizo pamoja na kujiongezea kipato.

Aidha Dkt. Ndugulile amezitaka Hlmashauri nchini kuhimiza wanawake na vijana kujiunga katika vikundi vya kijasiriamali ili kuwawesha  kupata mikopo ya kufanya biashara na miradi mbalimbali kama wanavyofanya wanawake na vijana wa wilaya ya Ludewa.

Dkt. Nduguile amewapa moyo wanawake na vijana hao wa wilaya ya Ludewa katika harakati za kutafuta kazi na kuwasihi vijana na wanawake wengine kutojibweteka wakisubiri ajira za kujiajiri bali wajiongeze na kujiajiri na hata kuajiri watu wengine.

"Jambo hili mnalofanya ni jambo jema la msingi litawasaidia kupata kipato na kujinua kiuchumi kwani kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya  Mhe.Rais Magufuli inasisitiza watu kufanya kazi hasa vijana na wanawake" alisema Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha DARE Bi. Theopista Mhagama amesema kuwa jumla ya vikundi 54 vimefanikiwa kujisajili katika Mamlaka mbalimbali ambazo zitawawezesha kuomba na kupata kazi za kutengeneza barabara na madaraja wilayani humo na Tanzania kwa ujumla

“Kwakweli tunafarijika sana kwani tumeamua kwa dhati kujikwamua kiuchumi na sio kukaa na kulalamika na kusbiri kufanyiwa kila kitu na Serikali wakati kama vijana na wanawake tunaweza kufanya kazi tukajiajiri na kuajiri wengine” alisema Bi. Theopista.

Ameongeza kuwa mpaka sasa wamepata kandarasi ya kujenga madaraja madogo katika barabara ya lwilo mbongo na yamefika katika asilimia 75 na wamedhutu kuomba tenda za ujenzi wa barabara na madaraja  za kitaifa kwani wanakidhi vigezo kama wakandarasi wengine.


No comments

Powered by Blogger.