Rais Magufuli Ameagiza Makontena ya Dhahabu yaliyozuiwa mwaka 2017 Yauzwe
Rais wa Tanzania dkt. John Magufuli ameagiza makontena ya mchanga wa dhahabu ambayo yalizuiliwa bandarini yasisafilishwe kwa mwaka 2017 yatafutiwe mteja na yauzwe kwa faida ya kampuni mpya ya Twiga ambayo ni muungano wa hisa za Serikali na za kampuni ya Barrick ili kuanza ukurasa mpya wa biashara.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Januari 24, 2020 baada ya kutiliwa saini mkataba wa makubaliano baina ya Serikali na kampuni ya madini ya Barrick Ikulu jijini Dar es salaam.
“Namnunuzi namjua, Kwa sasa huyo mnunuzi kama anataka kuja kununua anunue kwasababu tunajua faida itakayo patikana kwaajili ya kampuni yote (Twiga), tuendelee kushirikiana kwaajili ya faida ya pande zote mbili” amesema Rais Magufuli.
Machi 2017, baada ya Rais John Magufuli kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye dhahabu kwenda nje ya nchi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilizuia makontena 262 yenye mchanga huo uliokuwa katika Bandari ya Dar es Salaam kusafirishwa.

Hata hivyo,taarifa ya Tume ya Rais ya Uchunguzi chini ya Prof. Mruma iliyowasilishwa Mei 24, 2017, Imebainisha kuwepo kwa udanganyifu mkubwa wa kiwango cha madini yaliyopo kwenye mchanga na thamani halisi.
, kwa kutumia viwango vya wastani thamani ya mtali/madini yote katika makinikia ni TZS bilioni 829.4 na TZS bilioni 1,438.8 kwa kutumia viwango vya juu.
Katika hatua nyingine ,Rais Magufuli amesema kuwa alikuwa anaumia kuona dhahabu inasombwa na wananchi wanaambiwa ni mchanga wakati wakazi wa eneo ambalo kuna migodi wanaishi maisha duni.
Pia, ameagiza kuwa kampuni ya Twiga kuhakikisha wanahifadhi mazingira na kuwasaidia wakazi wa karibu na maeneo ya migodi pale wanapohitaji misaada ya kimaendeleo kama kuwajengea visima vya maji.
No comments
Post a Comment