Rais wa Marekani Donald Trump Katoa Hotuba Yake Baada ya Shambulizi la Iran
Rais wa Marekani Donald Trump Katoa Hotuba Yake Baada ya Shambulizi la Iran lililopiga ngome mbili za Marekani leo...Hapa Nimekuwekea Mambo Muhimu Sita aliyosema
1.Trump: Hatuko Tayar na Hatutakubali Iran imiliki Silaha za Nuclear
1.Trump: Hatuko Tayar na Hatutakubali Iran imiliki Silaha za Nuclear
2.Trump: Mashambulizi ya Iran hayajasabisha madhara yoyote. Hakuna Mwanajeshi hata mmoja aliyeuawa zaidi ya uharibifu mdogo tu kwenye kambi zetu
3.Trump: Iran wanaonekana kunywea; Makusudi kabisa wamechagua kutoua mwanajeshi wetu hata mmoja. Hii ni kitu kizuri kwetu na Dunia nzima
4.Trump: Jenerali wao tuliyemuua alikuwa anapanga kufanya mashambulizi makubwa kwenye ngome zetu, lkn tukamuwahi na kumuua.
5.Trump: Tunaomba washirika wetu wote wajitoe kwenye makubaliano ya Nuclear na Iran ili tutengeneze Makubaliano mapya yatakayoifanya Dunia nzima kuwa salama. Iran haipaswi kumili Silaha za Nuclear!
6.Trump: Marekani kwa sasa haihitaji mafuta au gesi toka Mashariki ya kati. Tunajitosheleza kwa kila kitu
Baada ya Trump kumaliza hotuba yake ya Dk 10 kuhusu Iran, hajaruhusu maswali na badala yake ametangaza kuiwekea Iran vikwazo zaidi kutokana na shambulizi la leo
Kwa mujibu wa picha za Setilaiti, Irani imerusha makomboa 22 leo na kupiga kambi mbili za Marekani ambapo majengo 5 ya kambi kubwa ya jeshi la Marekani ya al Asad Air Base yanaripotiwa kuharibiwa vibaya.

No comments
Post a Comment