Header Ads

Header ADS

Samatta waaga rasmi KRC Genk

    Mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mtanzania, Mbwana Samatta amewaaga wachezaji na viongozi wa timu hiyo tayari kwa safari yake kwenda kucheza Ligi Kuu England ‘Premier League’.

 Samatta anatajwa kuwaniwa na Norwich City inayoshiriki katika Premier league ikidaiwa kuwa imeweka mezani dau la pauni milioni 11 (Sh bilioni 33).
   “Samatta sasa hivi hayupo Ubelgiji ameshaaga rasmi wachezaji, viongozi na mashabiki juu ya suala la usajili wake wa kwenda kucheza England kwa sababu klabu zinazohitaji huduma yake ni nyingi.
   “Pia,alitakiwa aondoke muda sana isipokuwa wakala wake wa awali alikuwa akimsubirisha na muda unapotea, baadaye ndipo akabadili wakala, ambapo tayari kuna ofa ya hao Norwich, pia kuna West Ham na Brighton ni jambo la kusubiria kuona itakuaje,” alisema mzee Samatta    

No comments

Powered by Blogger.