Header Ads

Header ADS

TANZANIA YAPOKEA MSAADA KUTOKA SWEDEN ILI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

                Serikali ya Tanzania imetia saini mikataba miwili ya msaada na Serikali ya Sweden kwa kupatiwa dola milioni 90 sawa na Tsh. bilioni 240.95 kutoka Mfuko wa Ushirikiano wa Elimu Duniani, GPE
TANZANIA YAPOKEA MSAADA KUTOKA SWEDEN ILI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James ameitaja miradi husika kuwa ni Tsh. bilioni 88.55 zitakazogharamia Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) 2016/17 – 2021/2022 ikiwemo Elimu ya Msingi, Elimu Jumuishi, Elimu ya Watu Wazima na iliyo nje ya Mfumo Rasmi
Bilioni 116.40 zitaongeza mchango wa Serikali ya Sweden katika Program ya Elimu kwa matokeo (EPforR) lengo likiwa ni kuwezesha mpango wa maendeleo ya Sekta ya Elimu 2016/17 – 2021/22 hususan kuwezesha ubora na usawa katika matokeo ya Elimu ya Msingi na Sekondari

No comments

Powered by Blogger.