Header Ads

Header ADS

Zaidi ya nyumba 120 zimebomoka Wilayani Bahi Mkoani Dodoma.

   Zaidi ya nyumba 120 zimebomoka na madaraja kuharibika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ivi karibuni.
   Maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo ni , Uhelela, Laloi, Mugu na Nagulo  Bahi Sokoni, Bahi Misheni, Mji mpya, Nkogwa na, Mbuyuni.
 
   Aidha,Juzi Mkuu wa Wilaya, Mwanahamisi Mukunda akiongozana na wataalamu wa Halmashauri ya Bahi na watendaji wa vijiji, walitembelea baadhi ya wakazi walioathirika na mafuriko hayo na madaraja ambayo yameharibika.
   Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kijiji cha Sokoni, Sifael Mbeti alisema mvua imesababisha mito mingi kufurika na hivyo kusababisha maji kuleta madhara kwa kubomoa nyumba na madaraja.
    Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bahi Sokoni, Fredrick Kachiwile alisema zaidi ya nyumba 86 katika kijiji hicho zimebomoka.
  Pia.alisema katika Kijiji cha Uhelela taarifa za awali zinaonyesha nyumba 35 zilibomoka na katika Kijiji cha Nagulo barabara imekatika na mawasiliano ni ya shida.
  Mwenyekiti wa Kijiji cha Nagulo, Ashery Silla alisema jumla ya nyumba 18 zimeanguka.

No comments

Powered by Blogger.