JWTZ yakabidhiwa mitambo, magali ya mabilioni
Serikali ya Marekani, jana imekabidhi msaada wa magari na mitambo kwa jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania (JWTZ) yenye thamani ya dola za Marekani milioni 18.
Msaada huo umekabidhiwa na kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Petterson kwa Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi na kushuhudiwa na Mkuu wa majeshi ya ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika kituo cha mafunzo ya kulinda amani, Kunduchi.
Dkt. Inmi ametoa pongezi kwa Tanzania na kusema ni miongoni mwa nchi sita Afrika ambao ni wabia na Marekani katika kulinda amani Duniani, ambapo nchi nyingine ni Ethiopia, Uganda, Rwanda, Senegal na Ghana.
” Naipongeza Tanzania kuwa kinara wa amani kwani barani Afrika inashika nafasi ya tano na duniani inashika nafasi ya 11, na imekuwa ya kwanza kujitoa kulinda amani katika nchi za Sudan, Afrika ya kati, DRC na Lebanon” amesema Dkt. Inmi.
Waziri wa ulinzi, Dkt. Mwinyi ameishukuru Marekani kwa masaada huo na kusema unakuwa chachu kwao kuongeza juhudi za kulinda amani na kuzifikia nchi nyingi zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya ulinzi , Jenerali Mabeyo amesema ” Tanzania na Marekani ni kitu kimoja, tunashukuru wametupatia vifaa na kutoa mafunzo namna ya kutumia kabla ya kukabidhiwa”
Msaada huo ni magari 27 ya kubeba askari na mengine ya kubeba mizigo ya kisasa yenye uwezo wa kujikwamua yenyewe yakikwama.
Aidha kuna mitambo ya kupakua na kupakia mizigo, jiko linalotembea lenye uwezo wa kuhudumia watu 300, mashine za kusafisha maji na kuwa maji salama pamoja na mitambo ya mawasiliano ya kisasa.
No comments
Post a Comment