Kamanda wa jeshi la polisi usalama Barabarani apiga marufuku ukaguzi wa mabasi na malori kufanyika Barabarani.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim amepiga marufuku ukaguzi wa mabasi na malori kufanyika barabarani.
Kamanda huyo ameagiza taarifa za safari za basi na abiria waliopo kusainiwa na dereva na si wakala.
"Ni marufuku kwa wakala wa basi lolote kusaini vitabu vya taarifa lazima vitabu vyote visainiwe na madereva,” amesema.
Ametaka ufanyike kabla ya kuanza safari, mwisho wa safari, katika vituo vya mabasi vya Mikoa na Wilaya, kusisitiza kuwa ukaguzi wa malori ufanyike kwenye mizani.
Ameeleza hayo leo Jumamosi Februari Mosi, 2020 katika kikao cha pamoja kati ya kikosi hicho, Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), Chama cha Madereva (Uwamata) na wadau mbalimbali.
Akiwa katika stendi ya mabasi ya mikoani ya Ubungo (UBT), Muslim amesema ukaguzi wa mabasi utafanyika mwanzoni na mwisho wa safari pamoja na kwenye vituo vilivyopo katika wilaya na mikoa.
"Kulikuwa na malalamiko mengi na wengine mkatishia kugoma baada ya kukaa na viongozi wenu tumekubaliana mambo mbalimbali likiwemo basi kutosimamishwa na kufanyiwa ukaguzi barabarani," amesema Kamanda MuslimKamanda huyo ameagiza taarifa za safari za basi na abiria waliopo kusainiwa na dereva na si wakala.
"Ni marufuku kwa wakala wa basi lolote kusaini vitabu vya taarifa lazima vitabu vyote visainiwe na madereva,” amesema.
No comments
Post a Comment