Kocha mkuu wa Yanga ajipa matumaini juu ya Timu yake.
Kocha Mkuu wa Yanga,Luc Eymael amesema kuwa anaamini vijana wake watafanya makubwa ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2019/20 kutokana na uwezo walionao.
Timu ya Yanga inajiandaa kushuka uwanjani kesho, Mkwakwani Tanga kumenyana na Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Yanga ilisepa na pointi tatu baada ya kushinda bao 1-0 lililopachikwa kimiani kwa kichwa na Abdulaziz Makame akimalizia pasi ya kichwa ya Ally Ally.
"Huwezi kusema kwamba muda wa vijana wangu kupambana umekwisha hapana ni suala la muda tu kuona namna gani tutapata matokeo, nina imani uwezo wa vijana wangu ni mkubwa na tutafanya vema,".
No comments
Post a Comment