Header Ads

Header ADS

Magari Mawili Yagongana Na Kusababisha Majeruhi Na Uharibifu Jijini Mbeya

     Mnamo tarehe 17.02.2020 majira ya saa 03:00 usiku wa kuamkia leo huko eneo la Ilomba, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya – Tunduma, Gari lori tanker la mafuta lenye namba za usajili T.720 DHV na Tela T.520 CCY likiendeshwa na ABUBAKAR MOHAMED [32] Mkazi wa Dar es Salaam likitokea Dar es Salaam kuelekea nchini Zambia likiwa limebeba mafuta Petrol na Diesel liligongana uso kwa uso na Gari ndogo yenye namba za usajili T.536 DDM aina ya Toyota Carina iliyokuwa inatokea Mbeya Mjini.

    Katika ajali hiyo dereva wa gari ndogo T.536 DDM Toyota Carina amejeruhiwa na anaendelea na matibabu. 
   Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa magari yote mawili katika eneo la makazi ya watu.
   Aidha katika ajali hiyo magari yote mawili yameharibika na Tanker la Mafuta liliacha njia na kwenda kugonga maduka ya bidhaa mbalimbali yaliyopo kando kando ya barabara.
   Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama lipo eneo la tukio kuhakikisha mafuta yaliyopo katika gari lililopata ajali yanahamishiwa kwenye gari lingine bila kusababisha madhara yoyote ikiwa ni pamoja na jitihada za kuliinua tanker la mafuta lililoacha njia na kupinduka.

No comments

Powered by Blogger.