Makatibu wakuu wa CCM wameitikia wito wa kamati ya maadili na usalama wa Chama hicho.
Makatibu Wakuu Wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Yusuf Makamba na Ndg. Abdulrahaman Kinana leo Februari 10, 2020 wamefika katika Ofisi Ndogo za CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam kuitikia wito wa Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili inayoongozwa na Ndg. Philip Mangula.
Makatibu Wakuu hao Ndg. Abdulrahman Kinana na Ndg. Yusuf Makamba wamefika katika Ofisi hizo majira ya mchana na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally Kakurwa.
No comments
Post a Comment