Mfanyabiashara apigwa faini mil.9 kwa kukosa mashine ya EFD
Mamlaka ya mapato TRA, Mkoa wa Ruvuma imemtoza faini ya shilingi milioni 9 mfanyabiashara anayesambaza pembejeo kwa wakulima kwa kosa la kuuza mbolea bila kutumia mashine ya kutolea risiti ya EFD kama sheria inavyotaka.
Pia, kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa amesema jeshi hilo linamshikilia mfanyabiashara huyo kwa kosa la kuuza mbolea kinyume na bei elekezi ambapo urea ilipaswa kuuza kwa shilingi 54,500 lakini yeye anauza kwa shilingi 60,000 Januari 23 mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo alifanya ziara kwenye maghala ya kuuzia mbolea kwa lengo la kujua kama wanafuata bei elekezi ya serikali.
No comments
Post a Comment