Header Ads

Header ADS

Mhe,Mavunde amefungua Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko lililoandaliwa na UVCCM Mkoni Shinyanga.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenye ulemavu, Anthony Mavunde amefungua Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.











Kongamano hilo limefunguliwa leo Jumamosi Februari 1,2020 katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya shughuli za Chama Cha Mapinduzi kuelekea Miaka 43 ya CCM ambapo wananchi wameelezwa fursa mbalimbali za kuwezesha wananchi kiuchumi.

Mhe. Mavunde amewataka wananchi wa Shinyanga kuchangamkia zilizopo mkoani Shinyanga ili waweze kubadili maisha yao.
"Ndugu zangu fursa hazina mataili,haiwezi kukufuata. Haya maisha siyo ya tatu mzuka,changamkieni fursa zilizopo zilizopo.Tumieni elimu mtakayopata katika Kongamano hili kubadili hali ya maisha yenu",alisema Mavunde.

Kwa Upande wake ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliwataka wajasiriamali na wafanyabiashara kujitangaza badala ya kujifungia ndani kwa kisingizio cha kukosa masoko.

"Tumieni vyombo vya habari kutangaza bidhaa zenu,tumieni mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zenu badala ya kujifungia ndani.Lakini pia halmashauri zinatoa mikopo,naomba muombe mikopo hii ambayo haina riba ili muweze kuinuka kiuchumi",alisema Mboneko.

Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele aliwataka vijana kuishi kwa upendo,kushirikiana,kupendana na kuheshimiana ili kutimiza malengo yao.

No comments

Powered by Blogger.