Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe anyimwa na Mahakama ya mkazi Kisutu kibali cha kusafiri Nje ya Nchi.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemnyima mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kibali cha kusafiri nje ya Tanzania.
Amesema wakati mahakama ikitoa uamuzi huo, Spika Job Ndugai amemruhusu kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kusafiri.
Mwenyekiti wa Chama hicho aliomba kibali cha kusafiri katika nchi za Marekani, Uingereza na Uswisi kuanzia Februari 2 hadi 12, 2020 kwa shughuli binafsi na biashara.
Akizungumzia na waandishi wa habari leo Ijumaa Februari 7, 2020 mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema Mbowe alitakiwa kufungua shauri la kuomba kibali lakini amewekewa masharti mengi.
Amebainisha kwamba masharti aliyopewa ni kuwasilisha pasi yake ya zamani ya kusafiria, kwamba aliwasilisha nakala za hati yake mpya ya kusafiria zilizothibitishwa na wakili lakini zilikataliwa kwa madai kwamba imeanzia Septemba na mawakili wa Serikali wanataka ya zamani.
"Leo Mbowe amewaagiza mawakili wake kuondoa shauri la kuomba kibali kwa sababu amecheleweshwa safari yake," amesema Mrema na kueleza kusikitishwa na nguvu ya Mahakama kumezwa na mawakili wa Serikali.
Pia,Mrema amesema hiyo siyo mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kuzuiwa, kwamba viongozi wakuu wa chama na wajumbe wa kamati kuu ya Chadema walizuiwa na Mahakama katika safari yao ya Januari 13 hadi 17, 2020 kwenda Nairobi, Kenya kwa ajili ya mkutano unaohusu uchaguzi mkuu.
Hivyo,Mbowe na wenzake wanane wanakabiliwa na kesi namba 112 ya mwaka 2018 katika Mahakama ya Kisutu.
No comments
Post a Comment