Header Ads

Header ADS

Paul Kagame na Mseveni wafanya Mapatano ya kukabidiana waharifu.

  Mawaziri wa maswala ya kigeni wa Rwanda na Uganda wametia saini makubaliano ya kukabidhiana wahalifu wanaotafutwa na mataifa yote mawili katika mkutano uliofanyika katika mpaka ukisimamiwa na marais wa mataifa hayo mawili
  Mkutano huo uliunga mkono kuachiliwa kwa makumi ya raia waliokuwa wakizuiliwa kutoka pande zote mbili katika kipindi cha wiki chache zilizopita.
Kagame na Museveni wakutana mpakani Gatuna
Hali ya wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili imekuwepo kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusababisha mpaka wa Gakuna upande wa Rwanda kufungwa hatua ilioathiri raia na biashara.
 Sababu moja ya hali ya wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili imekuwa lawama zinazohusiana na maswala ya kiusalama.                                                                                  Rwanda imeshutumu Uganda kwa kuwahifadhi waasi wanaokabiliana na serikali ya taifa hilo huku Uganda ikimlaumu jirani yake wa kusini kuingilia vikosi vyake vya usalama.             Uganda sasa imekubali kuchunguza na kubaini madai ya Rwanda kwamba waasi wa Rwanda wamekuwa wakisajili na kufanya mafunzo.
  Pia imekubali kuzuia tatizo kama hilo kufanyika tena ndani ya ardhi yake.                       Mkutano huo ulikubali kwamba wakati hilo litakapoangaziwa , mkutano mwengine utafanyika katika kipindi cha siku 15 ili kuufungua mpaka huo.                                                 Hata hivyo,Hali ya wasiwasi kati ya viongozi hao wawili inaonekana kupungua.

No comments

Powered by Blogger.