Rais wa zamani wa Kenya, Daniel arap Moi, anazikwa leo Kabarak
Rais wa zamani wa Kenya, Daniel arap Moi, anazikwa leo kwenye mji wa nyumbani kwake wa Kabarak baada ya maelfu ya watu kushiriki jana ibada ya kutoa salamu za mwisho mjini Nairobi
Mwili wa Moi uliwasili Kabarak mapema leo asubuhi na Rais Uhuru Kenyata wa Kenya anatarjiwa kuongoza mamia ya watu kushiriki mazishi yake yatakayofanyika mchana wa leo.
Pindi ibada ya taifa hapo jana Rais Kenyata alimwelezea Moi kuwa kiongozi mpenda amani, baba wa taifa na kinara wa kupigania bara la Afrika pamoja na haki ulimwenguni.
Moi aliyeiongoza Kenya tangu mwaka 1978 hadi 2002 alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa mika 95.
Pia, utawala wa Moi aliyefahamika kwa jina la "Profesa wa Siasa" uliandamwa na visa vya rushwa na tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa haki wa za binaadamu.
No comments
Post a Comment