Header Ads

Header ADS

Wananchi wahama Makazi yao Baada ya Ziwa kujaa Maji

  Kaya 91 katika kijiji cha Bassotu wilayani Hanang mkoa wa Manyara zimezingirwa na maji hali iliyosababisha wayahame makazi yao baada ya Ziwa Bassotu kufurika.
  Hali hiyo imeilazimu jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kuifunga kwa muda  bara bara kuu inayounganisha mawasiliano kati ya Bassotu-Katesh na Singida kwa ajili ya Usalama wao na vyombo vyao vya moto.

  Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Basotu, Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara Paul Kasabago, amewataka Viongozi wa eneo hilo kuchukua tahadhari kwa kuwalinda watoto wanaokwenda shule hadi hali itakaporejea kawaida.
  Baadhi ya Wananchi wakizungumza na kituo hiki wamesema kwa sasa afya zao zipo hatarini kwa sababu wanatumia maji yaliyochanganyikana na maji taka baada ya vyoo kujaa maji.
  Hata hivyo,Diwani wa kata ya Basotu Samwel Qaoga amesema hali kama hiyo haijawahi kutokea katika miaka ya karibuni na kwamba walishachukua tahadhari mapema.
   Mtendaji wa kata hiyo Elizabeth Issalo amesema Kutokana na  hali hiyo mashamba yameharibiwa ovyo huku nauli zikiongezeka maradufu kutokana na mzunguko wa safari kuwa mkubwa .
   Mojawapo ya  nyumba zilizokumbwa na athari hizo ni pamoja na ya Mbunge wa Viti maalum (CHADEMA) mkoa wa Manyara Mheshimiwa Rose Kamili .

No comments

Powered by Blogger.