Watu 20 wafariki wakigombea mafuta ya upako mjini Moshi
Watu 20 wamekufa jana Jumamosi Februari Mosi, 2020 baada ya kukanyagana katika harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa mjini Moshi, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.
Taarifa zaidi za tukio hilo zinadai waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.
Taarifa zaidi za tukio hilo zinadai waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.
No comments
Post a Comment