Marekani kutoongeza muda wa kukaa karantini
Rais donald Trump wa Marekani amesema hataongeza muda wa miongozo ya watu kujitenga (karantini) baada muda wake uliopangwa Alhamisi hii kumalizika.
Pamoja na kukabiliana na upinzani kutoka pande tofati za taifa hilo, Rais Trump amesema serikali haitazidisha muda wa mwisho wa raia wake kujitenga kutokana na janga la Corona.
Hata hivyo watu wake wa karibu akiwemo mshauri wake, Jared Kushner, wametabiri kwamba Marekani ambayo ipo katika hali mbaya ya kimaambukizi kwa wakati huu, hali hiyo inaweza kujirudia tena Julai.
Wakati hayo yakijiri, huko Japan kwa hivi sasa waziri Mkuu Shinzo Abe anatarajiwa kuwasiliana na wataalamu kutathimini uwezekano wa kuongeza muda wa tangazo la hali ya hatari.
Mpaka hivi sasa Japan ina maambukizi 14,119 na vifo 435, lakini Marekani ina maambikizi milioni 1.05 vifo vikiwa vimefikia 61,472.
No comments
Post a Comment