Marekani yasimamisha ufadhili wa Shirika la Afya Duniani [WHO]
Ikiwa Mmarekani ni mfadhili mkuu katika Shirika la Afya Duniani [WHO] .Rais Trump ameshutumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
"China ina mamlaka yote kwenye Shirika la Afya Duniani ," rais alisema hayo wakati akitangaza hatua ambazo zilipaswa kuchukuliwa dhidi ya China.
Marekani ni mfadhili mkubwa wa shirika hilo la afya, lakini ufadhili huo kwa sasa utaenda kwenye mashirika mengine sasa, alisema.
Marekani ni mfadhili mkubwa ambaye alichangia zaidi ya dola milioni 4000 kwa mwaka 2019.
Bwana Trump, ambaye anafanya kampeni za kuwania kuchaguliwa tena kuwa rais amekuwa akikosolewa kwa namna anavyokabiliana na mlipuko wa corona, na amekuwa akiilaumu China kwa kuficha taarifa za mlipuko huo wa virusi vya corona.
Zaidi ya watu 102,000 nchini Marekani wamepoteza maisha kutokana na Covid-19 na taifa hilo ndio limetajwa kuwa na takwimu kubwa zaidi ya vifo vilivyosababishwa na corona duniani kote.
"Leo tutasitisha uhusiano wetu na Shirika la Afya Duniani na kuhamisha ufadhili tunaotoa hadi kwenye mashirika mengine ya afya", Bwana Trump alisema akiwa White House katika bustani ya Rose.
"Dunia inahangaika sasa hivi kwa sababu ya makosa ya serikali ya China," alisema.
Aliongeza kuwa China imesababisha maisha ya Wamarekani zaidi ya 100,000 kupotea kutokana na mlipuko huo wa virusi.
Rais Trump ameishutumu China kwa kullipotosha shirika la afya duniani WHO kuhusu virusi.
No comments
Post a Comment