Rais wa Afrika Kusini ametehadharisha kuwa hali ya mlipuko wa virusi vya corona inaelekea kuwa mbaya zaidi, wakati akitangaza kulegeza masharti ya kubaki nyumbani.Cyril Ramaphosa amesema zaidi ya watu 22,000 wamerekodiwa kuwa na maambukizi juma lililopita.Pamoja na hayo , rais amesema kuwa sharti la kutotoka nje halijaondolewa moja kwa moja.Alitangaza kuwa kuanzia tarehe 1 mwezi Juni, masharti zaidi yataondolewa.Bwana Ramaphosa alikuwa akizugumza baada ya kampuni ya madini nchini Afrika Kusini kusema kuwa wafanyakazi 164 katika mgodi wa dhahabu karibu na ji wa Johannesburg wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.Nchi hiyo imethibitisha vifo vya watu 429 mpaka sasa kutokana na Covid-19.Sharti la kusalia nyumbani litalegezwa vipi? Sharti la muda wa kurejea nyumbani halitakuwepo tena, biashara zaidi zitaruhusiwa kuendelea na shule zitafunguliwa, Rais Ramaphosa alieleza.Marufuku ya biashara ya pombe itaondolewa kwa idadi maalumu ya mauzo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pekee na '' kwa masharti ya siku maalumu na saa maalumu'', ameeleza kiongozi huyo.Lakini Bwana Ramaphosa anasema marufuku ya biashara ya sigara itaendelea kuwepo ''kutokana na hatari za kiafya zinazotokana na uvutaji wa sigara''.Pia amesema shule zitafunguliwa kwa awamu kwasababu ''tunazingatia maendeleo ya watoto wetu na kizazi chote cha watu wanaojifunza hawapaswi kuwa waathirika wa kudumu wa janga hili''.Lakini alisema kuwa ''hakuna mzazi atakayeshurutishwa kumpeleka mtoto shuleni kama watakuwa na wasiwasi kuhusu usalama wao shuleni''.Alisema nini kuhusu kuenea kwa virusi? Ramaphosa amekuwa kwenye shinikizo kubwa akitakiwa kulegeza masharti ili kuufungua tena uchumi.Hatahivyo, ameutahadharisha Umma kuwa hali itakuwa mbaya siku za usoni.''Tutarajie kuwa idadi ya watu walioambukizwa itaongezeka zaidi na kwa haraka,'' alisema.''Janga la corona nchini Afrika Kusini litakuwa baya zaidi kabla ya hali kuwa nzuri,'' aliongeza.Kuna uwezekano wa takriban watu 40,000 kupoteza maisha nchini humo ifikapo mwishoni mwa mwaka, wanasayansi walitahadharisha juma lililopita.
No comments
Post a Comment