Header Ads

Header ADS

Magufuli achukua fomu ya kugombea uraisi 2020

   Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dkt, John Magufuli, leo   17,Juni amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa na chama chake kushiriki katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.
      Magufuli amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally kwenye Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dodoma.


   Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Dkt Magufuli amesema anaanza mapema mchakato wa kutafuta wadhamini  ili awahi kurejesha fomu hiyo mapema.

Mwenyekiti huyo wa CCM amesema amekuwa akipigiwa simu na makada wa chama hicho, ambao wamemuahidi kumdhamini.

“Naomba nianze zoezi hili la kutafuta wadhamini, nitaenda mikoa yote kwa sababu nimekuwa nikipigiwa simu wakisema wanataka kunidhamini hivyo nitarejesha fomu yangu kwa wakati,” amesema Magufuli.

No comments

Powered by Blogger.