Msimu wa Championship kuanza Juni 20
Msimu wa championship umepangwa kuanza tarehe 20 Juni, miezi zaidi ya mitatu baada ya kuahirishwa kwasababu janga la virusi vya corona.
EFL ilisema tarehe ni "awali" na "itatekelezwa iwapo masharti yote ya usalama na kanuni za muongozo wa serikali zitatimizwa".
Kuna mechi 108 zilizosalia, pamoja na michezo ya kupanda daraja ya nusu na fainali.
Hakuna michezo ya Championi iliyopangwa ambayo imekwishachezwa tangu tarehe 8 Machi kutokana na kwamba michezo iliahirishwa siku tano baadae.
EFL imesema kuwa imeazimia kukamilisha msimu wa Championi kwa fainali za mtoano " tarehe au karibu na tarehe 30 Julai", na kuongeza kuwa kutakua na mazungumzo yatakayoendelea juu ya mapendekezo ya kuruhusu matumizi ya wachezaji mbadala katika mechi zilizosalia zilizopangwa na kuongeza vikosi vya siku za mechi kuanzia wachezaji 18 hadi 20.
Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya Serikali ya Uingereza kuruhusu mashindano ya michezo nchini humo kufunguliwa tena ndani ya majengo, kuanzia Jumatatu.
Mashindano ya farasi na snooker kila mmoja itafufua mashindano yake, huku Primia Ligi ikijhtarajiwa kuanza tarehe 17 Juni.
"Kufuatia tangazo la Jumamosi la serikali la kuruhusu matukio ya michezo kuanza ndani ya majengo, EFL wikiendi hii imeafiki kutoa tarehe ya awali ya kuanza tena michuano yake tarehe 20 Juni 2020 kwa machi katika Sky Bet Championship," iliandikwa taarifa ya EFL.
"Baada ya kujadili mbinu kadhaa na umuhimu wa kukamilisha msimu katika kipindi kilichopangwa sawa na kile cha Premia Ligi ili kuepuka tatizo linaloweza kujitokeza kwa timu zilizodhaminiwa na klabu zilizopandishwa daraja , msimu wa Sky Bet Championship umepanga kukamilika kwa mechi za fainali za mtoano karibu au siku yenyewe ya tarehe 30 Julai 2020."
No comments
Post a Comment