Serikali ya Burundi imezindua operesheni ya upimaji mkubwa wa maambukizi ya COVID-19 katika mji mkuu wa kibiashara wa nchi hiyo Bujumbura. Bw. Ndikumana pia amesema, operesheni hiyo imechagua mji wa Bujumbura kutokana na kuwa maambukizi mengi ya COVID-19 yametokea mjini humo.Waziri huyo pia amesema serikali inapanga kuanza upimaji kwenye maeneo mengine kabla ya Ijumaa, wakianza na maeneo ya miji mikuu ya mikoa. Tokea mwezi Machi, ni watu 3,000 pekee waliopimwa COVID-19 nchini Burundi na miongoni mwao watu 191 walipatikana na ugonjwa huo. Kwa mujibu wa takwimu rasmi ni mtu mmoja tu aliyefariki huku asilimia 80 ya walioambukizwa wakiruhusiwa kuenda nyumbani baada ya kupata matibabu hospitalini.
No comments
Post a Comment