Header Ads

Header ADS

Chama cha CCM chatoa siku 14 kwa Viongozi wa Wilaya na Mikoa kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM

       Kupitia kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza viongozi wa chama hasa kupitia Kamati za Siasa katika ngazi za wilaya na mikoa ndani ya siku 14 wakamilishe kukagua miradi yote ya maendeleo ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika maeneo yao na taarifa ya kilichojiri iwasilishwe ofisini kwake.

     Kutokana na maagizo ya kuwataka kukagua miradi ya maendeleo, Chongolo pia amewaagiza kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa ilani na amesisitiza kuwa chama kitafuatilia utekelezaji wa maagizo hayo.
   Katibu huyo Mkuu wa Chama  ametoa maagizo hayo  mkoani Morogoro wakati akikagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa  (SGR), akiwa ameambatana na Wajumbe wa Sekreterieti ya Chama Taifa.


"Niwapongeze watu wa Morogoro kwani mmeweza kuonesha njia nami nimeamka nije hapa na sekretarieti yangu kujionea kama kinachofanyika hapa ni kile kilichoelekezwa katika ilani yetu ya uchaguzi na ndicho kinachoelezwa kila mara,"amesema Chongolo na kuongeza "Haya ni maagizo na maelekezo Kama tulivyopeana mara baada ya mkutano mkuu maalum kuwa wote tushuke chini kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo yetu ."

Amesema wao wanawajibu wa  kuisimamia Serikali na utekelezaji wa Ilani kwani ni sisi ndio tutakaorudi kuwaeleza wananchi nini tumefanya.

Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa amesema anaishikuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa wakati kwa ajili ya kukamilisha mradi huo huku akifafanua mpaka sasa wamelipa  hati 34 kati ya 35 huku hiyo moja ambayo inalipwa muda wowote kuanzia sasa.

No comments

Powered by Blogger.