Header Ads

Header ADS

Mahakama yaahirisha Kesi inayo mkabili mheshimiwa Freeman Mbowe Mpaka kesho

 kutokana na muonekano hafifu wa video conference, kesi hiyo imeahirishwa mpaka kesho tarehe 06/08/2021 .Ambapo Mbowe  kesho atafikishwa mahakamani majira ya saa 3:00 asubuhi.

Kesi hiyo ya ugaidi ilikuwa itajwe leo Agosti 5, 2021, ambapo Mbowe na wenzake walikuwa katika Gereza la Ukonga Dar es Salaam lakini kutokana na matatizo ya mtandao ilishindwa kuendeshwa vizuri.

Akizungumza hii leo mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala, amesema kuwa, "Teknolojia imefeli hivyo tumeshindwa kufanikisha mchakato huo kwa sababu kumekuwa na mawasiliano hafifu kati ya video conference facility za hapa katika Mahakama ya Kisutu na Gereza la Ukonga na tumekubaliana kwamba kesho washtakiwa waletwe mahakamani," ameeleza Wakili Kibatala

No comments

Powered by Blogger.